Michezo

Real Madrid yaanza vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya

0
Real Madrid Ligi ya Mabingwa Ulaya
Real Madrid wakisherekea Ushindi dhidi ya Ajax

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid imeanza vizuri mbio zake za kutetea taji hilo baada ya kuifunga Ajax kwa mabao 2-1 katika hatua ya 16 bora.

Ajax walicheza vizuri na walifanikiwa kupata bao lililofungwa na Nicolas Tagliafico, lakini matumizi ya kifaa cha kusaidia kutoa uamuzi cha VAR kilisababisha mwamuzi kulikataa bao hilo.

Mabingwa watetezi Real Madrid walipata uongozi wa mchezo baada ya kufunga bao kupitia kwa Karim Benzema aliyepiga shuti lililojaa pembeni ya kona ya juu ya goli baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Vinicius Jr.

Hakim Ziyech alisawazisha baada ya kupiga shuti kutoka umbali wa kama meta 10 lakini Marco Asensio aliifungia Real Madrid bao la ushindi akiunganisha wavuni krosi ya Dani Carvajal.

Timu hiyo ya Uholanzi ilicheza vizuri mchezo huo lakini bahati haikuwa yao, huku Dusan Tadic akikaribia kufunga baada ya shuti lake kugonga mwamba katika kipindi cha kwanza na David Neres, ambaye alitengeneza bao la Ziyech, alipiga shuti mikononi mwa kipa Thibaut Courtois katika moja ya nafasi za wazi za kufunga.

Soma pia:  Arsenal yakaribia kumsajili Ceballos

Kasper Dolberg aliyeingia akitokea benchi, anusura afunge katika dakika za majeruhi wakati alipoteleza wakatia kipiga mpira ndani ya boksi, huku kipa Courtois akifanikiwa kuzuia mpira huo.

VAR NOMA KWA AJAX

Teknolojia hiyo ya VAR ambayo ndio imeanza kutumika katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu huu katika hatua ya mtoano ndio ilikuwa jambo kubwa katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Johan Cruyff Arena.

Ajax nusura wapate bao la kuongoza wakati Tagliafico wakati alipopiga mpira kwa kichwa ilipotokea piga nikupige katika lango la Real Madrid.

Kona ya Lasse Schone ilimkuta Matthijs de Ligt, ambaye mpira wake wa kichwa ulimpita hewani Courtois.

Lakini baada ya kuwasiliana na mwamuzi msaidizi wa video, mwamuzi wa kati Damir Skomina alikwenda kuangalia tena tukio lile katika skerini na kuamua sio goli.

Soma pia:  Higuain matumaini yote kwa Sarri

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kubaini kuwa mshambuliaji wa Ajax Tadic alikuwa katika nafasi ya kuotea mbele ya Courtois hasa pale alipokuwa akipiga kichwa.

Kiufundi ulikuwa uamuaiz sahii, hatahivyo kama kusingekuwa na VAR, basi bao lile lingekuwa halali.

Zidane ameondoka, na aliyembadili Julen Lopetegui alitimuliwa na sasa Santiago Solari ndiye mtu aliyechukua nafasi, lakini wameweza kushinda Ulaya licha ya kutocheza vizuri.

Real imeshinda mechi sita kati ya saba za ugenini za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika hatua ya mtoano, ikishinda kila mechi ya hatua ya nne bora.

Ajax haijashinda katika mechi zake sita za hatua ya mtoano za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya nyumbani, ambapo kwa mara ya mwisho walishinda Machi mwaka 1996 dhidi ya Borussia Dortmund.

Soma pia:  Gareth Bale kubaki Madrid

Karim Benzema wa Real Madrid amefunga au kusaidia kupatikana kwa bao katika kila michezo sita ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya walipocheza dhidi ya Ajax (mabao manne, na kusaidia mara nne).

Hakuna mchezaji yeyote wa La Liga aliyefunga mabao zaidi kuliko Benzema wa Real Madrid mwaka 2019 katika mashindano yote (mara nane, akiwa sawa na Lionel Messi).

Vinicius Jr amesaidia mara nane katika mashindano yote kwa Real – ikiwa ni zaidi ya mchezaji mwingine yeyote.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo