Michezo

Manchester United na PSG kushitakiwa

0
Manchester United na PSG kushitakiwa
Mechi ya Man United dhidi ya PSG jumanne

Klabu za Manchester United na Paris St-Germain zimeshtakiwa na Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) kufuatia vurugu katika mchezo wao wa hatua ya 16 bora wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya uliofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumanne.

Man United imeshitakiwa baada ya mashabiki wake kutupa vitu uwanjani na kuwazuiwa wafanyakazi wa uwanjani kufanya majukumu yao.

PSG wenyewe wamestakiwa kwa kuwasha mafataki wakati wa mchezo huo, kurusha vitu na kufanya usumbufu.

PSG ambao ni mabingwa wa Ufaransa walishinda mchezo huo wa kwanza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa katika kipindi cha pili na Kimpembe na Kylian Mbappe.

Kesi hiyo itasikilizwa na Kamati ya Maadili na Nidhamu ya Uefa Februari 28. Kabla ya kuanza kwa mchezo huo, mashabiki wa PSG walipua fataki kwenye uwanja huo wa Old Trafford.

Soma pia:  Paul Pogba amkubali sana Kocha Solksjaer

Kutokana na tukio hilo, inaelezwa kuwa viti karibu 800 upande wa timu ngeni viliharibika na kusababisha hasara.

Mshambuliaji wazamani wa Manchester United Angel di Maria alitupiwa chupa wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo.

Polisi wa Manchester walithibitisha kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa lakini kuna mtu aliondolewa na wahudumu baada ya chupa kutupwa uwanjani hapo.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo