Top Stories

Russia yawatimua wanadiplomasia wa Marekani

0
russia yawatimua wanadiplomasia
Picha: Vladimir Putin (kushoto) na Theresa May (kulia)

Russia yawatimua wanadiplomasia 60 wa marekani na kufunga ubalozi uliopo St.Petersburg, Ikiwa ni majibu kwa kitendo cha Marekani kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia.

Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov. Uamuzi wa Marekani ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Russia kudaiwa kuhusika katika shambulio dhidi ya jasusi wa zamani wa Russia, Sergei Kripal.

Hadi sasa zaidi ya nchi 20 za Ulaya zimefukuza wanadiplomasia wa Russia katika kuiunga mkono Uingereza. Lavrov alisema nchi nyingine zilizowafukuza warusi wasubiri majibu kwa vitendo.

Aliongeza kuwa ubalozi wa Marekani umepewa taarifa juu ya hatua hiyo kama majibu kwa Marekani kwa kuwatimua wanadiplomasia wake.

Baada ya hatua hiyo Msemaji wa Marekani, Heather Nauert, alisema Russia haina nia ya kuwa na uhusiano mzuri na nchi nyingine, hivyo Marekani ina haki ya kuchukuwa hatuia nyengine dhidi ya taifa hilo.

Soma pia:  Museveni awalaumu wanasiasa Uganda

“Russia imeamua kujitenga zaidi yenyewe, tunaangalia maamuzi ya kuchukua”. aliwambia waandishi wa habari.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, Kripal bado yupo kayika hali mbaya hospitalini lakini binti yake ambaye naye aliwekewa sumu anaendelea vizuri.

Kutokana na kuhusishwa kwa Russia na tukio hilo Uingereza ilisema hawatatuma mawaziri wake pamoja na familia ya malkia kushiriki kombe la dunia.

Itakumbukwa kuwa mwaka 1989 Rais wa MarekaniRonald Reagan, aliwatimua wanadiplomasia 80 wa Russia.

Mwaka 2016 uongozi wa Marekani, Barack Obama, uliwafukuza wanadiplomasia 35 wa Russia baada ya kudukua taarifa za chama cha Democratic.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories