Baada ya Raila Odinga Kujiapisha siku ya jumanne kama ni Raisi wa Watu katika Viwanja vya Uhuru Park, Nairobi, Kenya. Raila ameunga orodha ya viongozi wa Kiafrika ambao waliojitangaza wenyewe kuwa maraisi ingawa nchi zao tayari zina Kiongozi.
Viongozi wa 4 kutoka Afrika waliowahi kujiapisha wenyewe;
1. Mashood Abiola
Mwanasiasa ambaye pia alikuwa Mfanyabiashara Mkubwa nchini Nigeria, Aliwania kiti cha Uraisi katika uchaguzi uliofanyika Juni 12, 1993. Na alifanikiwa kushinda Uchaguzi mkuu lakini hata hivyo Mkuu wa Jeshi Ibrahim Babangida, alitisha uchaguzi mwengine, uamuzi huo ulipelekea machafuko ya kisiasa.
Mwaka 1994 Abiola Alijitangaza mwenyewe kuwa ni Raisi halali wa Taifa la Nigeria eneo la Epetedo katika Kisiwa cha Lagos. Na baadae akakamatwa na Kufungwa kwa miaka 4.
Abiola Alifariki Julai 7, 1998 katika hali ya Utata baada ya kuwachiliwa Huru
2. Ettiene Tshisekedi
Alikuwa Kiongozi mkuu wa Upinzani kwa mda mrefu, Tshisekedi alijitangaza mwenyewe kuwa kiongozi aliyehaguliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati alishindwa katika uchaguzi Mkuu wa 2011 na Raisi Joseph Kabila.
Baadaye alikamatwa na kuweka chini ya ulinzi, Kabla ya kufariki Feburuari 1, 2017 akiwa katika matibabu huko Brussels, Ubelgiji.
3. Jean Ping
Mwaka 2016, Kiongozi huyo wa Upinzani nchini Gabon, alijitangaza mwenyewe kuwa Raisi na kuomba kuhesabiwa tena kwa kura ambazo zimethibitisha Raisi Ali Bongo kuwa ameshinda uchaguzi.
Ping Alihakikisha kuwa Ulimwengu wote unajua kama yeye ni Raisi ingawa ilisababisha machafuko makubwa katika Mji wa Libreville na miji mingine nchini Gabon mpaka kusababisha uharibifu kwa bunge.
4. Kiiza Besigye
Baada ya kupoteza dhidi ya Raisi Yoweri Museveni kwa mara nne mfululizo. Baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa Februari 2016, Kiiza Besigye aliamua kujiapisha kwa siri katika eneo lisilofahamika siku moja kabla ya Sherehe za kuapishwa rasmi kwa Raisi Museveni, Alikamatwa haraka na kuwekwa katika kizuizi na kufikishwa Mahakamani baadae, Kesi yake bado inaendelea ingawa sasa yuko nje kwa dhamana.
Comments