Top Stories

Saudia Arabia yakabidhi tani 100 za tende

0
Saudia Arabia yakabidhi tende Zanzibar
Tende Zanzibar

Serikali ya Saudia Arabia imeikabidhi msaada wa tende tani 100 Serikali ya Zanzibar kwa ajili ya kuwapatia wananchi mbalimbali wa visiwani humo Zanzibar.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Ofisi ya Wizara ya Katiba na Sheria na kuhudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Khamis Juma Mwalim na mwakilishi wa Serikali ya Saud Arabia, Zyad Abdullah Abdullah Abuhasbu.

Akizungumza baada ya makabidhiano ya tende hizo, Waziri Mwalim, alisema wizara yake itahakikisha inasimamia ugawaji wa tende hizo kwa walengwa waliotarajiwa.

Alisema Serikali ya Saudia Arabia imekuwa na uhusiano mzuri wa kidugu na Zanzibar na kutoa misaada mbalimbali ya kimaendeleo.

“Tunawashukuru sana ndugu zetu wa Saudia Arabia kwa misaada yao wanaotupatia, uhusiano wetu ni wa historia na wa muda mrefu,” alisema.

Soma pia:  Ligi ya ZFA Zanzibar kukosa Wadhanini

Vile vile, aliiomba serikali ya Saud Arabia kuendelea kuisaidia Zanzibar katika huduma ya upatikanaji wa majisafi na salama.

Naye Mwakilishi wa Balozi wa Saudia Arabia, Abuhasbu, aliishukuru Serikali ya Zanzibar kwa ushirikino wao na kukubali kupokea msaada huo kwa ajili ya wananchi wa Zanzibar.

“Huu msaada wa tende umeletwa na wananchi wa Saudia Arabia kwa ajili ya ndugu zao wananchi wa Zanzibar kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya nchi mbili hizi,” alisema.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories