Top Stories

Trump asaini mpango wa dharura kujenga ukuta

0
Trump kujenga ukuta
Trump baada ya kuweka saini mpango wa dharura wa kitaifa.

Rais wa Marekani, Donald Trump amesaini mpango wa dharura wa kitaifa ili kupanua ukuta wa mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Kusainiwa kwa mpango huo kumetimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za urais, kuwa akichaguliwa atajenga ukuta wa mpaka kati ya mataifa hayo mawili.

Hatua hiyo inampa madaraka ya kujipatia fedha uamuzi ulioibua maswali kisheria.

Akitetea hatua hiyo, Trump alisema atasaini dharura ya kitaifa, kwani wanavamiwa na watu wanaoingiza dawa za kulevya, magenge ya wahalifu na watu wa kawaida.

Ikulu ya Marekani imepanga kuelekeza fedha zilizotengwa kwa mambo mbalimbali ili kujenga ukuta huo na hadi sasa Dola bilioni 8,zimepatikana za kujenga ukuta huo.

Awali Rais Trumph alihitaji Dola bilioni 5.7 Wakizungumza hatua hiyo, Spika wa baraza la chini la bunge, Nancy Pelosi na kiongozi mwenye viti vichache bunge la juu, Chuck Schumer wameiita hatua hiyo ya Trump si ya halali na kutupilia mbali kauli yake ya kuwepo msukosuko katika mpaka.

Soma pia:  Floyd Mayweather Macho yake kwenye fedha

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories