Nchini Sudan imetangaza rasmi kufunga mipaka yake na nchi ya Eritrea wiki moja baada ya Raisi wa Sudan, Omar Al Bashar alivyotangaza hali ya dharura ya miezi sita katika mikoa ya Kassala na North Kurdufan, shirika la habari la serekali la SUNA lilisema Jumamosi.
Shirika la SUNA halikutoa sababu za kufungwa kwa mpaka huo.
“Gavana wa Kassala, Adam Gemaa Adam, alitoa amri inayoagiza kufungwa kwa mipaka yote na nchi ya Eritrea, kulingana na amri ya urais … ambayo ilitangaza hali ya dharura huko Kassala,” SUNA ilisema.
Wakazi watatu wa Kassala waliiambia shirika la Reuters kwamba askari walikuwa wakitumika karibu na mpaka. Msemaji wa kijeshi hakuweza kufikiwa kwaajili ya kutoa maoni.
“Uamuzi huo ulianza rasmi siku ya Ijumaa mda wa jioni”, Shirika hilo la SUNA liliongeza.
Comments