Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga anatarajia kujiapisha leo katika viwanja vya Uhuru Park.
Sherehe hio ya kuapishwa kwa kiongozi upinzani watu inatarajiwa kuanza saa 2:30 asubuhi na kumaliza saa 7 mchana.
Wabunge na wageni waalikwa wanatarajiwa kufika saa 3 asubuhi na Viongozi wakuu wa NASA wanatarajiwa kuwasili saa4 asubuhi katika viwanja hvyo vya Uhuru Park.
Jeshi la Polisi kwa upande wake linaonya vikali kuhusu kutokea kwa sherehe hizo za kumwapisha kiongozi wa upinzani kwani ni kinyume na katiba ya Kenya pia ni kitendo ambacho kitahatarisha amani ya taifa hilo lakini NASA wanasisitiza kuwa mipango yao itaendelea licha ya onyo kutoka kwa Mkuu wa polisi Nairobi, Japheth Koome.
Comments