Michezo

Ligi ya ZFA Zanzibar kukosa Wadhanini

0
Ligi ya ZFA Zanzibar
Ligi ya ZFA Zanzibar

Uongozi wa Kamati ya kusimamia mashindano na ligi ya ZFA Taifa umesema, suala zima la udhamini bado hawajalipatia dawa hasa kutokana na mfumo wa ligi ulivyo.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hussein Ali Ahmada alisema, wanafahamu kwamba hivi sasa ni vigumu kupata udhamini katika hali waliyo nayo ikiwemo utitiri wa klabu na chama chenyewe kinachosimamia masuala ya mchezo huo kutokutulia.

Hivyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo ni mapema kuwapata Wadhamini.

Alisema hivyo, kama kamati, wakati huu wanajaribu kutafuta watu wa kuwasaidia ili kuendesha mambo yao na kufika hatua ya kuwa na mifumo mizuri.

“Kimsingi kama sisi kamati kasoro nyingi zilizojitokeza tumeweza kuziona ni kasoro ambazo ni za kawaida kwa sababu mambo mengi yaliyokuwa yakijitokeza uwanjani ni malalamiko kwa waamuzi,”, alisema.

Soma pia:  Kamati ZFA Zanzibar yasubiri ripoti ya waamuzi

Alisema hali hiyo ni ya kawaida kwa sababu wanafahamu mpira wa Zanzibar ulivyokuwa mwanzo na walivyohamasisha makundi mbalimbali kujitokeza viwanjani.

Alisema, hali hiyo ilianza kupungua kidogo kidogo baada ya kuwa na timu nyingi.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo