Michezo

Klopp: Liver haitatumia fedha nyingi kusajili

0
Liver haitatumia fedha nyingi kusajili
Kocha Jurgen Klopp

Kocha Jurgen Klopp amesema kwamba Liverpool bado iko sokoni kwa ajiili ya kusaini wachezaji wapya, lakini amebainisha hawatatumia kiasi kikubwa cha fedha.

Klopp bado hajaongeza mchezaji yoyote katika kikosi chake msimu huu zaidi ya beki kinda wa Uholanzi, Sepp van den Berg.

Manchester City na Tottenham zote zimevunja rekodi zao za usajili kipindi hiki cha majira ya joto, lakini Klopp amesema kuwa hana hofu ya Liverpool kutoongeza wachezaji wapya na amesisitiza kuwa ana furaha na kikosi chake.

“Sio rahisi,” amesema Klopp akiiambia televisheni ya Liverpool. “Nilisema mwaka jana kwamba, kuimarisha timu sio kitu rahisi. Hatuwezi kutumia fedha nyingi, ingawa bado tupo sokoni.

“Sisi sio klabu ambayo inatumia fedha nyingi. Hatuwezi kufanya hivyo. Ni ukweli kwamba ni matajiri, lakini hatuwezi kufanya kama wengine wanavyofanya. “Lakini bado tupo sokoni. Tutaangalia nini cha kufanya, lakini kikosi changu bado kipo imara.

Soma pia:  Sarri ataka Juventus imsajili Danny

“Kuna wakati mwingine kusajili wachezaji wapya siyo suluhisho, tuna wachezaji wengi kikosini mwetu na wao ndio wanatakiwa kuwa suluhisho letu.”

Comments

Comments are closed.

More in Michezo