Michezo

Arsenal yakaribia kumsajili Ceballos

0
Arsenal yakaribia kumsajili Ceballos
Dani Ceballos

Arsenal inakaribia kuthibitisha kumsajili kwa mkopo kiungo wa Real Madrid, Dani Ceballos.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania chini ya umri wa miaka 21 atatangazwa wakati wowote ndani ya saa 24 kutua Arsenal kwa mkopo wa muda mrefu na wamewapiku wapinzani wao wa jiji la London, Spurs kuchukua nyota huyo wa Real Madrid.

Arsenal pia imemsajili beki wa kati, William Saliba mwenye umri wa miaka 18 kutoka St Etienne, ambaye jana alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya.

Kocha wa Arsenal, Unai Emery amesema: “Tunazungumzia uwezekano wa kumsajili tena mchezaji mmoja kwa mkopo. Tuna majina tofauti. Klabu inalifanyia kazi hilo. “Ceballos ni mchezaji mzuri. Namjua tangu akiwa Real Betis na baadaye akatua pale Real Madrid”.

Soma pia:  Klopp: Liver haitatumia fedha nyingi kusajili

Unai Emery aliongezea kwa kusema “Alicheza vizuri mno katika timu ya taifa ya Hispania chini ya umri wa miaka 21, ambapo timu yake ilishinda kwenye mashindano. “Ni mchezaji ambaye atakuwa msaada mkubwa kwetu na nina imani kubwa kwamba ataisaidia timu msimu ujao.”

Comments

Comments are closed.

More in Michezo