Michezo

Manchester United yakaribia kumsajili Dybala

0
Manchester United yakaribia kumsajili Dybala
Paulo Dybala

Klabu ya Juventus itakubali kumuuza mshambuliaji wake, Paulo Dybala kwa Manchester United katika kipindi hiki cha majira ya joto endapo mahitaji yao yatafikiwa na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.

Thamani ya mshambuliaji huyo imetajwa kuwa ni kati ya pauni milioni 70 na 90 na klabu yake haitakuwa tayari kukaa mezani ili kujadili uhamisho wa Dybala endapo hakuna ofa rasmi yoyote ambayo imewasilishwa.

Ole Gunnar Solskjaer anamhitaji zaidi mchezaji huyo ambaye pia anaichezea Timu ya Taifa ya Argentina ilikuongeza nguvu katika kikosi chake baada ya kuwapo kwa mchakato wa Romelu Lukaku na Paul Pogba kutajwa wanataka kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi cha majira ya joto.

Kocha huyo wa United anaamini kwamba ana idara nzuri ya ulinzi ambayo itatumika kupenya katika ngome za wapinzani na endapo watafanikiwa kumnasa mchezaji huyo, atamtumia kama mchezaji wa mbele ambaye atakuwa na jukumu la ushambuliaji.

Soma pia:  Bale azigonganisha Real Madrid na Inter Milan

Licha ya United kukutana na ushindani katika vita ya kuwania saini ya mchezaji huyo dhidi ya Paris Saint-Germain na Inter Milan, ingawa inaelewa kuwa Dybala anatarajia kujiunga hapo baadaye.

Huku Maurizio Sarri tayari akiwa ameshaweka wazi mipango aliyokuwa nayo kwa ajili ya msimu ujao, lakini ameamua kubatilisha uamuzi wake kwa kumwondoa Dybala kwenye mipango yake ya kukitumikia kikosi hicho.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea alikuwa ameshamwondoa Dybala katika mipango yake ya ndani na nje kwenye idara ya kupachika mabao, kama alivyokutana na hali hiyo kwa Dries Mertens alipokuwa Napoli.

Na kwa wakati huo huo, Sarri hajaonekana kukata tamaa kufuatia uamuzi huo wa kumuuza Dybala uliofanywa na Juventus atafurahi kuona kama itatumia fedha itakazopata kwa ajili ya kusajili mchezaji mwingine ambaye ana kipaji katika nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo