Michezo

Mambo 10 huenda ulikuwa huyafahamu kuhusu Ronaldo

0
Mambo 10 huenda ulikuwa huyafahamu kuhusu Ronaldo
Cristiano, Ronaldo

1) AMENZA SOKA 2002

Ronaldo alianza kucheza soka la kulipwa Agosti 14, 2002, akiwa Sporting, Klabu ya Ureno. kipindi hiko alikuwa na umri wa miaka 17.

2) MFUNGAJI  BORA KATIKA HISTORIA YA MADRID

Cristiano Ronaldo ameweza kufunga jumla ya magoli 427 katika Mechi 421 Alizochezea katika Klabu ya Real Madrid, Wachezaji wengine waliowahi kuchezea Madrid na kufunga mabao mengi ni Di Stefano, Raul, Puskas na Santillana

3) HAJAFUNGA KATIKA MASHINDANO MAWILI TU ALIYOSHIRIKI

Cristiano Ronaldo amecheza Ureno, Uingereza na Hispania, na ameweza kushinda katika mashindano yote alioshiriki isipokuwa Community Shield na Ligi ya Europa.

4) DOUBLES 99

Mshambuliaji huyo amefunga Jumla ya Double (magoli mawili kwa mechi. 99 katika ulimwengu wa Soka. ambapo 73 alifunga akiwa na Real Madrd, 25 akiwa na Manchester United na moja akichezea Sporting ya Ureno.

Soma pia:  Gareth Bale kubaki Madrid

5) MFUNGAJI BORA WA URENO

Ronaldo ni amefunga jumla ya mabao 79 katika Mechi 147 alizowahi kucheza akiwa na Timu yake ya Taifa ya Ureno.

6) AMESHINDA MARA TANO BALLON D’OR

Ronaldo anaungana sambamba na Messi, na ndio wachezaji pekee walioshinda mara nyingi tunzo hio, ambapo ameshinda tuzo hizo mara tano, mara mbili za mwisho kwa mfululizo.

7) AMESHINDA TUZO YA MFUNGAJI BORA UEFA MARA 6

Tangia msimu wa mwaka 2007/2008, ambapo alinda tunzo ya mfungaji bora wa UEFA, akiwa na Manchester United. Ronaldo aliendelea kushinda tunzo hio mara 5 mfululizo akiwa na Real Madrid kwanzia msimu wa mwaka 2012/13

8) AMEFUNGA MAGOLI 61 KATIKA MSIMU MMOJA

Katika msimu wa mwaka 2014/15, Ronaldo aliweza kufunga magoli mingi zaidi (61), ambapo alipita idadi ya magoli 60 aliyofunga katika msimu wa mwaka 2011/12.

Soma pia:  Real Madrid wakomaa na Pogba

9) AMEANZA KUCHEZA KIMATAIFA AKIWA NA MIAKA 17

Ronaldo alianza kuwakilisha taifa lake katika michuano ya Kimataifa akiwa na miaka 17, ambapo mechi yake ya kwanza alicheza dhidi ya Kazakhstan.

10) AMETUMIA NAMBARI NNE TOFAUTI ZA MGONGONI

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid, amekuwa akionekana sana kutumia jezi namba 7 lakini haimanishi ndio namba pekee aliyowahi kuvaa mgongoni. Hapo kabla aliwahi kuvaa jezi namba 17, 9, na 28

Comments

Comments are closed.

More in Michezo