Klabu ya Manchester United ilipata kipigo chake cha kwanza ikiwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer baada ya kufungwa 2-0 na PSG katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Kocha huyo tangu aichukue timu hiyo Desemba mwaka jana kutoka kwa mtangulizi wake aliyetimuliwa, Jose Mourinho, ambaye alishindwa kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri.
Baada ya mechi hiyo dhidi ya PSG, wachambuzi mbalimbali wakiwemo wachezaji nyota wa zamani na wadau wengine wa soka wamejadili kipigo hicho na nafasi ya Manchester United katika mchezo wa marudiano utakaofanyika mwezi ujao.
PHILI NEVILLE ANENA
Beki wa zamani wa Manchester United, ambaye anashikilia nafasi ya 10 kwa kuicheza mechi nyingi katika Ligi Kuu ya England, alisema kuwa timu yake hiyo ya zamani haina matumaini ya kuvuka hatua hiyo ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kutokana na kipigo hicho.
“Sifikiri kabisa kama Manchester United ina nafasi yoyote ya kufanya vizuri jijini Paris (katika mchezo wa marudiano dhidi ya PSG).
Beki huyo aliendelea kuimwagia sifa timu hiyo na kusema kuwa, PSG ina nyota kibao Ulaya, tena wale wa viwango vya juu kabisa na wanaoheshimika barani humo.
Ingawa hatukumuona Mbappe katika kiwango chake cha ubora, lakini alicheza vizuri katika mchezo huo na ni mmoja wa wachezaji waliofunga goli na kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kujiweka katika mazingira mazuri.
Ole Gunnar Solskjaer alikiita kipigo hicho cha Manchester United kama ni cha kusikitisha lakini alisisitiza kuwa pamoja na ugumu uliopo, “lakini Mlima uko pale kwa ajili ua kupanda.”
Winga wa zamani wa Man United, Angel di Maria alisaidia kupatikana kwa mabao hayo yaliyofungwa na Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe.
KOCHA AZUNGUMZA
Kocha wa muda wa Manchester United, Solskjaer alisema: “Kamwe huzi kukaa chini na kukata tamaa ukisema kuwa imekwisha”.
Manchester United wanatakiwa kujiandaa vizuri ili kuhakikisha wanapindua matokeo na kuweka hai kampeni zao za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kipigo hicho kutoka kwa Paris St-Germain kwenye uwanja wa Old Trafford.
Hiko ni kipigo cha kwanza kwa kwanza kuonjwa na Ole Gunner Solskjaer tangu kocha huyo ajiungwe na Manchester United.
Mbali na mabao ya Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe kuiweka Man United katika nafasi ngumu, na kutolewa nje kwa Paul Pogba nako kumeiongezea mzigo Man United licha ya kuwa mwenyeji katika mchezo huo wa kwanza. KOCHA WA PSG Kocha wa PSG, Thomas Tuchel anasema: “Angel di Maria ni mchezaji mwenye ushindani mkubwa katika soka wakati wote wa mchezo.
“Nafikiri alikuwa na uhusiano mzuri pamoja na mashabiki. Kiasi fulani kama alichanganyikiwa lakini ilibidi kuwa mtulivu katika kipindi cha kwanza. Mwishoni alifanikiwa kufanya vizuri.” ‘TULIKUWA WAZURI’ Beki wa PSG, Kylian Mbappe alisema: “Watu waache kujenga hofu na kuogopa. “Bila shaka, Neymar ni muhimu sana na Cavani ni msingi kwetu, lakini soka linachezwa uwanjani. Hilo tumelidhihirisha juzi.
Tumeonesha hilo. Hakuna kuogopa, tuko vizuri.” ‘Kwa kweli timu yetu haimuogopi yeyote katika mashindano’. Kiungo wa zamani wa Manchester United, Owen Hargreaves alisema kilikuwa kipindi kizuri kwa PSG, kwani walicheza vizuri licha ya kutokuwa na wachezaji wao wawili wanaowategemea.
Tangu msimu uliopita katika kikosi chao walimuongeza kipa wa kiwango cha dunia Buffon na katika kikosi cha mtaalam wa ufundi Tuchel. Ikiwa watakuwa na Cavani na Neymar hawamuhofia yeyote katika mashindano. “Tunajenga kitu fulani kizuri,” alisema Herrera.
Ander Herrera ambaye ni kiungo wa Manchester United alisema mchezo ulikuwa 50- 50 hadi pale ilipopigwa kona. Baada ya bao la kwanza kwa kweli kila kitu kilibadilika. Mchezo ulikuwa sana na ungeweza hata kumalizika kwa suluhu, kama wasingefunga kutokana na kona.
“Nafikiri tulipoteza mwelekeo [wakati Antony Martial na Jesse Lingard walipotoka nje baada ya kuumia katika kipindi cha kwanza] lakini tulifanikiwa katika muunganiko fulani pamoja na Alexis Sanchez na Juan Mata…” Mbappe wa PSG anakuwa mchezaji watatu kufunga katika mechi tatu za ugenini za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya England, baada ya Luis Enrique na Edin Dzeko.
Wakati Mbrazili Neymar ana muda mrefu wa kukaa nje ya uwanja, mwenzake wa Uruguay Cavani yeye atakuwepo wakati wa mchezo wa marudiano ya timu yake ya PSG itakaporudiana na United jijini Paris, Ufaransa Machi 6.
Comments