Top Stories

Watu 17 wafa moto hotelini India

0
Watu 17 wafa moto hotelini India
Hoteli ya Arpit Palace

Watu 17 wamekufa katika ajali ya moto uliozuka katika hoteli ya Arpit Palace mjini Delhi India.

Taarifa ya polisi ilisema moto huo ulizuka jana asubuhi na miongoni mwa waliopoteza maisha, yumo mtoto na mama yake ambao walijaribu kujiokoa kwa kuruka kutoka dirishani.

Watu wapatao 35 waliokolewa kutoka ndani ya hoteli hiyo na majeruhi walikimbizwa hospitalini.

Vyombo vya habari vya nchini hapa vinasema vifo vingi vilitokana na ukosefu wa hewa. Video zilizorekodiwa na mashuhuda wa tukio zinaonesha baadhi ya watu wakiruka kutoka kwenye jengo hilo.

Mmoja wa waokoaji, Vipin Kenta, aliliambia gazeti la Hindustan Times kwamba watu walishindwa kutumia korido kutoka hotelini kwa sababu imejengwa kwa mbao.

Miongoni mwa waliookolewa ni pamoja na mgeni katika hoteli hiyo, Sivanand Chand (43) aliyesema alipotoka chumbani kwake, alisikia sauti kutoka vyumba vingine zikiomba msaada.

Soma pia:  Biashara yaongezeka kati ya Urusi na China

Chand alisema alifungua dirisha na kuona moto mkali ukiwaka na ndani ya muda mfupi chumba kiligeuka kuwa cheusi kutokana na moshi.

Alisema waokoaji walitumia takribani nusu saa kumfikia kwa kuwa ngazi haikufika kwenye gorofa aliyokuwa. Moshi mzito ulionekana ukifuka kutoka kwenye gorofa ya juu ya hoteli hiyo iliyoko katika eneo la Karol Bagh, lenye maduka mengi na hoteli za bei nafuu ambazo hupendelewa na watalii. Shughuli za uokozi zilidumu kwa takribani saa moja.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali za karibu. Naibu Kamishna wa Polisi, Mandeep Singh Randhawa alisema wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.

Waziri Mkuu, Narendra Modi ametuma salamu za rambirambi. Matukio ya moto yanatajwa kutokea mara kwa mara nchini hapa.

Soma pia:  Jeshi Marekani laua Al Shabaab 15

Desemba mwaka jana, watu sita walikufa baada ya moto kuzuka katika hospitali moja iliyopo Mumbai, jimbo la Maharashtra. Vilevile mwaka 2017 watu 14 walikufa baada ya mgahahawa mkubwa katika eneo la Mumbai kushika moto.

Wakati huohuo zaidi ya watu 100 wamekufa baada ya kunywa pombe ya kienyeji inayosadikiwa kuwa na sumu.

https://www.youtube.com/watch?v=d98nO–fW_Y

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories