Top Stories

Jeshi Marekani laua Al Shabaab 15

0
Jeshi Marekani laua Al Shabaab
Al Shabaab

Jeshi la Marekani limewaua wapiganaji 15 wa kundi la Al-Shabaab kupitia mashambulizi mawili ya anga Kusini mwa Somalia.

Kamandi ya Marekani ya Afrika (AFRICOM) inayosimamia vikosi vya Marekani barani Afrika ilisema shambulizi la kwanza la anga lilifanyika karibu na Gandarshe, Mkoa wa Lower Shebelle na kuua wanamgambo 11.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wapiganaji wanne wa al-Shabaab waliuawa katika shambulizi la pili la anga mwishoni mwa wiki karibu na Bariire katika Mkoa wa Lower Shebelle.

“Shambulizi hili la anga lilitekelezwa baada ya washirika wetu wa Somalia kuzingirwa na Al-Shabaab wakati wakiendesha operesheni ya kuharibu juhudi za Al-Shabaab waliokuwa wakiwatoza kodi isivyo halali na kuwatisha raia katika eneo hilo,” ilisema taarifa ya AFRICOM.

Soma pia:  Sera za Uhamiaji za Trump kumgusa 21 savage

Mkurugenzi wa Operesheni wa AFRICOM, Gregg Olson alisema katika taarifa hiyo kuwa, Serikali ya Shirikisho ya Somalia inaweka shinikizo kwa al-Shabaab na washirika wao, pia mazingira ya kuimarishwa usalama na utulivu.

AFRICOM ilisema hakuna raia aliyejeruhiwa au kuuawa katika mashambulizi hayo ya kutokea angani na kuahidi kuendelea kuisaidia Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kwa kusambaratisha wanamgambo.

Marekani inaendesha operesheni zake za kijeshi kuisaidia Somalia kwa miaka kadhaa hali iliyopelekea mashambulizi hayo kusababisha vifo kwa al-Shabaab miezi miwili iliyopita

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories