Top Stories

Waangalizi wa Urusi wazuiwa Ukraine

0
Waangalizi wa Urusi wazuiwa Ukraine
Picha na UNIAN

Bunge la Ukraine limepitisha muswada wa kuwapiga marufuku waangalizi wa Urusi kufuatilia uchaguzi ujao wa rais na wabunge. Bunge la nchi hiyo lilisema kuwa muswada huo ulipitishwa kwa kura 232 zaidi ya kura 226 ambacho ni kiwango cha chini kilichohitajika.

Imeelezwa sheria hiyo imepitishwa ili kuizuia Urusi isiingilie uchaguzi wa Ukraine na kuzuia mashambulizi ya taarifa ili kupotosha ukweli kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Ukraine.

Mwezi uliopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Pavlo Klimkin (pichani), alisema alituma barua Ofisi ya Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya (OSCE) inayohusika na Taasisi za Kidemokrasia na Haki za Binadamu (ODIHR), kuomba ikatae maombi ya Urusi ya kutaka kutuma ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi.

Soma pia:  Wabunge Venezuela wawekewa vikwazo

Urusi kupitia Wizara yao ya Mambo ya Nje, ilizilaumu mamlaka za Ukraine kwa hatua zilizo kinyume na demokrasia na uamuzi wa watu. Imeelezwa Desemba 31, 2018, Tume Kuu ya Uchaguzi ilitangaza rasmi kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa rais na siku hiyo hiyo, ilifunga vituo vya kupigia kura vilivyoko nchini Urusi.

Klimkin alinukuliwa akisema kuwa ingekuwa hatari kwa wananchi wa Ukraine kupiga kura kwenye uchaguzi wa rais wakiwa Urusi. Uchaguzi wa rais nchni humo umepangwa kufanyika Machi 31 mwaka huu na uchaguzi wa wabunge umepangwa kufanyika Oktoba 27.

Imeelezwa uhusiano kati ya Kiev na Moscow umeendelea kuzorota tangu mwanzoni mwa mwaka 2014 kutokana na mgogoro wa Crimea na migogoro ya kijeshi Mashariki mwa Ukraine.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories