Tanzania imejiunga na Kenya katika kupitisha pasipoti mpya za kieletroniki mwezi januari, 2018, baada ya Kenya kuanza kutoa pasipoti za kieletroniki mwezi septemba mwaka jana, na kuwa nchi ya kwanza katika Jumuiya ya Afrika mashariki kufanya hivyo.
Uganda, Rwanda and Burundi bado hazijaanza kutoa pasipoti za kielekroniki, lakini bado wapo katika hatua za kuhakikisha wanaaza kutoa pasipoti hizo mpya za kielekroniki
Rwanda wapo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa kugawa tenda juu ya kuanzisha mfumo huo mpya wa Pasipoti, huku wenzao Burundi tayari imeshapitisha mpango huo wa kutoa pasipoti za EAC za kielekroniki huku wakisubiri kuzizindua rasmi.
Uganda na wao bado wako katika hatua ya ununuzi na ufadhili wa kuanza kutoa pasipoti mpya za kielectoniki za EAC.
Pasipoti za Kielektroniki za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinakuza na rangi tatu ikiwa ni nyekundu, kijani na buluu ya mawingu, ambazo ni rangi ya Bendera za Jumuiya hio EAC.
Comments