Top Stories

Alsisi ashinda tena urais Misri

0
Alsisi ashinda tena urais
Adel Fattah Al-sisi, Rais wa Misri

Rais wa Misri Adel Fattah Al-sisi ashinda tena urais Misri kwa muhula wa pili. Kiongozi huyo alichaguliwa kwa asilimia 92 ya kura kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotangazwa jana.

Kwa mujibu wa magazeti yanayomilikiwa na serikali ya Al-Ahram na Akhbar el-youm pamoja na shirika la habari la MENA, watu millioi 23 walipiga kura kati ya watu millioni 60 waliorodheshwa kwenye daftari la wapiga kura.

Kulingana na Al-Ahram, kura hizo millioni 23 zilizopigwa kura millioni mbili 2 ziliharibika kutokana na wapia kura kuingiza majina ya wagombea ambao hawakuwa miongoni mwa wagombea wawili waliothibitishwa.

Mpinzani wa pekee wa Al-sisi alikuwa Moussa Mostafa Moussa, ambaye anawaunga mkono Rais Abdel Fattah Al-sisi, Moustafa Moustafa alijiandikisha muda mfupi kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi.

Soma pia:  Kukosa nidhamu kwaitoa Senegal Kombe la Dunia

Abdel Fatah Al-sisi, aliyekuwa mkuu wa majeshi alimwondoa madarakani Rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa, Mohammed Morsi, baada ya kufanyika maandamano makubwa ya mwaka 2013.

Al-sisi alishinda muhula wake wa kwanza mwaka 2014 kwa kupata asilimia 96.9 ya kura zote. Kuondolewa kwa Morsi kulisababisha uharibifu mbaya, huku mamia ya waislamu wenye msimamo mkali waliuawa.

Tume ya uchaguzi ya nchini Misri imeonya kwamba wale ambao hawataweza kuonyesha sababu nzuri iliyowafanya wasishiriki kwenye uchaguzi wanaweza kukabiliwa na faini ya pauni 500 za Misri.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Ofisa wa tume hiyo, Mahmud Al-sherif, alisema hakukuepo na ukiukwaji wa sheria ya uchaguzi.

Vikundi vya upinzani vilitoa wito wa kususia uchaguzi huo.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories