Michezo

Mwili wa Emiliano Sala wapatikana

0
Mwili wa Sala wapatikana
Watu mbali mbali wakitoa salama za mwisho kwa Emiliano Sala

Mwili uliopatikana katika mabaki ya ndege iliyoanguka baharini, umetambulika kuwa ni ule wa mchezaji mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala, Polisi ya Dorset imeeleza.

Sala, 28, alikuwa akisafiri kwenda Cardiff katika ndege iliyokuwa ikirushwa na rubani David Ibbotson, ambayo ilipoteza mawasiliano na baadae kuanguka Januari 21.

Mwili huo ulipatikana Jumatano jioni baada ya mabaki ya ndege hiyo kupatikana Jumapili asubuhi. Polisi wa Dorset walithibitisha kupatikana kwa mwili huo usiku wa juzi Alhamisi.

Katika tarifa yao polisi ilisema: “Mwili uliopatikana leo (juzi) Alhamisi Februari 7, 2019 umetambulika kuwa ni wa mwanasoka Emiliano Sala.

“Familia ya mchezaji huyo na ile ya rubani David Ibbotson wamekuwa wakipewa taarifa za mara kwa mara kuhusu habari hizi na wataendelea kusaidiwa.” Mwili huo ulipatikanakatika mabaki ya ndege hiyo na mamlaka waliweza kuupata mwili huo siku mbili baadae, licha ya changamoto kibao.

Soma pia:  Mwanafunzi Kutoka Tanzania Auwawa Afrika Kusini

Tawi la taasisi ya Uchunguzi wa Ajali za Anga (AAIB) lilisema zoezi badi linaeendelea nma familia zimekuwa zikipewa taarifa za mara kwa mara.

Ndege ya Malibu N264DB ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Ufaransa kwenda Cardiff, baada ya mwanasoka huyo wa Argentika kufanya safari ya ghafla akirejea katika klabu yake ya zamani ya Nantes baada ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 15 katika klabu yake mpya ya Cardiff, alipata ajali baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuanguka baharini.

Cardiff City, walitoa taarifa baada ya kuthibitishwa kwa mwili wa mchezaji huyo, wakisema: “Tunatoa masikitiko yetu kwa faimilia ya Emiliano. Yeye na David (rubani) kuwa wataendelea kuwemo katika mawazo yetu”.

Wachezaji mbalimbali nyota waliandika katika mitandao ya kijamii wakielezea masikitiko yao baada ya kuthibitishwa kupatikana kwa mwili wa mchezaji huyo, ambaye ada yake ni rekodi ya Cardiff kwa kutoa fedha nyingi kumsajili mchezaji mmoja.

Soma pia:  Simanzi, Kifo cha Godzilla
Kifo cha Emiliano Sala
Emiliano Sala

Comments

Comments are closed.

More in Michezo