Mwanafunzi wa Phd katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ) kutoka nchini Tanzania, Baraka Leonard Nafari aliuawa siku ya Ijumaa, Februari 23, 2018, taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii imeeleza.
Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, CCTV ya Chuo Kikuu hicho ilionyesha Marehemu na Wanafunzi wenzake wawili wa UJ wakikimbia kunusuru maisha yao huku wakifuatwa na watu wawili wakiwa na Taxi.
Taxi hiyo ilimgonga Bwana Nafari kwa makusudi dhidi ya uzio wa Chuo hicho kikuu cha Johannesburg, na kusabisha kifo chake, taarifa hio ilieleza.
Kwa mujibu wa taarifa hio, Licha ya maelezo yaliyotokana na video, dereva wa teksi alikamatwa kwa kuendesha gari bila ya leseni ambako aliachiliwa kwa dhamana, na mtu mwengine aliyekuemo katika Taxi pia aliachiliwa huru bila ya malipo.
“Baraka alikuwa ni Mtanzania na tulimkaribisha hapa. Tunasumbuliwa kuwa Chuo Kikuu, ambacho kinajivunia zaidi wanafunzi wake wa Kimataifa, lakini bado hakijatoa taarifa kwa umma kuhusiana na mauaji haya ya kutisha,” taarifa hio ilieleza zaidi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiani wa Mashariki mwa Afrika, Dkt Augustine Mahinga alisema kuwa ofisi yae haikufahamu ripoti kuhusiana na mauwaji hayo, na alisema kuwa atawasiliana na maafisa wa juu kwa lengo la kufanya uchunguzi ripoti hio kisha kutoa maelezo kwa umma.
“Kwa sasa, niko nje ya Ofisi na sijui taarifa yeyote kuhusiana na ripoti hiyo, lakini wacha niwasiliane na wenzangu na kuwahimiza kufuatilia taarifa hio na kutupatia taarifa zaidi.” alifafanua wakati akiwasiliana na The Citizen kwa njia ya simu siku ya Ijumaa, Machi 2, 2018.
Comments