Top Stories

Vodacom Mpesa yapewa tuzo Ivory Coast

0
Vodacom Mpesa yapewa tuzo Ivory Coast
Vodacom Mpesa

Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kupitia huduma yake ya M-pesa imetambuliwa na kupewa cheti cha ubora wa hali ya juu katika hudama za kifedha.

Tuzo hiyo ilitolewa jana katka Mji wa Abijan, Ivory coast imetambua usalama na nia thabiti ya M-pesa katika kulinda haki ya mteja.

Tuzo hiyo ilitolewa baada ya Vodacom Mpesa kufika vigezo vilivyowekwa na GSMA ambavyo ni viwango vya juu vya kulind amana ya mteja, usalama wa huduma, usiri, kulinda taarifa za wateja, kupambana na utakatishaji fedha.

Nyingine ni kupambana na wanaogharamia vikundi vya ugaidi, na kupambana na mbinu za udanganyifu.

“Utambuzi na cheti  hiki unathibitisha nia na utendaji wa Vodacom Tanzania katika kuhudumia na kulinda haki za mteja katika eneo lote la biashara ya M-pesa,” alisema lan Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom.

Soma pia:  Uganda, Rwanda, Burundi kuanza kutumia passport za kielektroniki

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories