Top Stories

Museveni awalaumu wanasiasa Uganda

0
Museveni awalaumu wanasiasa Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amewatupia lawama wanasiasa kutokana na mgogoro wa ardhi wa Apaa, akisema wanatia chumvi na kuchochea mgogoro huo.

Alisema lengo la wanasiasa hao aliowaita uchwara ni kutafuta umaarufu kwa kuwaingiza wananchi katika matatizo.

Akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki iliyopita Rais Museveni alisema mgogoro huo umekuwa mkubwa kutokana na viongozi dhaifu kushika hatamu ya kuongoza jamii ya eneo hilo kutafuta suluhu, wakati moyoni mwao wakitafuta ‘kiki’ ya kisiasa katika eneo hilo.

Baadhi ya viongozi katika wilaya za Amuru na Adjumani wanadaiwa kuchukua ardhi yenye rutuba katika eneo hilo na kuwagonganisha wananchi wa wilaya hizo wakafarakana na kuanza kupigana.

“Tatizo kuu katika mgogoro wa ardhi wa eneo la Apaa linasababishwa na viongozi dhaifu wanaotafuta umaarufu wa kijinga katika migongo ya wananchi wa Apaa,” alisema.

Soma pia:  Marekani yatakiwa kuondoka Syria

Mgogoro huo wa ardhi unaohusisha makabila ya Madi na Acholi kugombania ardhi yenye ukubwa zaidi ya kilomita za mraba 80, umesababisha watu zaidi ya watano kujeruhiwa na watu zaidi ya 2,100 kuachwa bila makazi baada ya nyumba zao kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

Rais Museveni aliwataka wasaidizi wake kufika katika eneo la tukio na kuwasikiliza wananchi kuanzia ngazi ya chini hadi wilayani ili kuwabaini wale wote waliohusika na uchochezi wa mgogoro mzima.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories