Top Stories

Marekani yatakiwa kuondoka Syria

0
Marekani yatakiwa kuondoka Syria
Jeshi la Marekani

Urusi imeitaka Marekani kutimiza ahadi yake ya kuondoa majeshi yake yote nchini Syria. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Sergei Ryabkov aliwaambia waandishi wa habari msimamo huo wa serikali yake.

“Tunasisitiza Marekani itimize ahadi yake na kujiondoa kabisa nchini Syria,”alisema.

Desemba 19 mwaka jana, Rais wa Marekani Donald Trump aliamuru majeshi ya nchi yake yote kuondoka Syria kwa madai kuwa Kikundi cha kigaidi cha IS kimeshaanguka.

Takriban wanajeshi 2,000 wa Marekani wapo Syria. Kwa mujibu wa maofisa wa Marekani, itachukua kati ya siku 60 na 100 wanajeshi hao kuondoka nchini humo.

Wakati huohuo, zaidi ya nyumba za makazi 31,000 zimekarabatiwa nchini Syria hadi Februari 10 mwaka huu. Mkuu wa Kituo cha Usuluhishi cha Urusi kilichopo Syria, Sergei Solomatin alisema pia shule 810 na vituo vya afya 137 vimekarabatiwa na kuanza kazi.

Soma pia:  Bunge Japan laidhinisha bilioni 28/- kukabili majanga

“Tunaendelea kusaidia kurudisha katika hali ya kawaida miundombinu na kuweka mazingira mazuri kwa wakimbizi kurejea. Tumeshakarabati barabara za urefu wa kilometa 999.8,”alisema.

Solomatin alisema tayari watu 221,883 wamesharejea nyumbani kwao na vituo 10 vya wakimbizi vinapewa msaada.

Kwa mujibu wa kituo hicho cha usuluhishi, zaidi ya wananchi 2,000 wameandamana katika mji wa Deir ez-Zor wakitaka majeshi ya Marekani yaondoke nchini humo.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories