Burudani

Tuzo za Grammy 2019 zapata pigo

0
Tuzo za Grammy 2019
Tuzo za Grammy 2019

Ikiwa leo zinafanyika tuzo za heshima za muziki za Grammy, imebainika kuwa nyota mbalimbali walikataa ofa ya kutumbuiza katika shoo ya hafla hiyo itakayofanyika kwenye Ukumbi wa Staples Centre, California.

Kwa mujibu wa Jarida la New York Times, limedadavua kuwa Drake, Kendrick Lamar na Childish Gambino walielezwa mapema kuhusiana na kupewa nafasi hiyo lakini wote walikataa pasipo sababu maalum.

Moja ya watayarishaji wa tuzo hizo, alieleza wanamuziki wengi hasa ‘weusi’ hujitoa kujishughulisha na tuzo hizo kila inapotokea wamekosa kutunukiwa tuzo katika msimu uliopita.

Mara kadhaa tuzo hizo zimekuwa zikishutumiwa kuwa na upendeleo kwa wasanii kadhaa.

Mwingine aliyejitoa katika orodha ya watumbuizaji ni mwimbaji wa Pop, Ariana Grande ikielezwa kuwa sababu ya kujitoa kwake ni baada ya kukatazwa kutumbuiza wimbo wake mpya wa 7 Rings.

Soma pia:  Trump asaini mpango wa dharura kujenga ukuta
Tuzo za Grammy 2019 drake
Drake, Kendrick Lamar na Childish Gambino

Comments

Comments are closed.

More in Burudani