Msanii anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya komedi, Peter Mollel ‘Piere Liquid’ amezidi kupaa Kimataifa baada ya kuonekana nchini Marekani kwa muendelezo wa shughuli zake za sanaa na mambo mengine ya kijamii.
Hatua hiyo ni baada ya lile shavu alilopewa hivi karibuni bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kusafiri na Timu ya Taifa ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenda nchini Misri kwenye michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Piere ameendelea kula mashavu na picha yake imepostiwa na kituo cha habari cha nchini Marekani inaonyesha ni jinsi gani riziki ya mtu anapotoa Mungu hauwezi kuiziba kwa fitna binafsi.
Awali kabla ya kula shavu la Marekani, viongozi mbalimbali wa serikali kwa nyakati akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na wengineo kwa nyakati tofauti walionesha kuguswa na mchango wa msanii huyo.
Comments