Top Stories

Kifusi chaua Mgodini Kitunda

0
Kifusi chaua Mgodini Kitunda
Mgodini kitunda

Mkazi wa kijiji cha Ipiriro, Wilayani Maswa, Mkoani Simiyu, Sangundi peter (18), amefariki dunia na mwenzake kunusurika, baada ya kuangukiwa na kifusi katika mgodini Kitunda ambao upo mkoani Tabora.

Diwani wa Kata ya Kitunda, Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora, Seif, alisema tukio hilo lilitokea siku ya Jumanne iliyopita, saa 5 usiku katika mgodi huo, baada ya vijana hao kuvamia eneo hilo ambalo siyo rasmi na kuchimba shimo refu pasipo kuchukua tahadhari.

Seif  alisema Pete na mwenzake walikuwa peke yao ndani ya shimo hilo wakichimba dhahabu kinyume na utaratibu.

“Vijana hao walikuwa hawatambuliki katika maeneo hayo na walikuwa wavamizi katika mashimo ambayo yalishafungwa na serikali, wao walikuwa wameingia usiku kwajili ya kujipatia dhahabu kwa njia ya wizi.” alisema Diwani seif

Soma pia:  Vituo vya TV vimefungiwa baada ya kurusha Raila akila kiapo

Diwani huyo alisema kutokana na tukio hilo, vijana wenzao walipo jaribu kuulizana kama wanawafahamu, wengi walionyesha kutowafahamu vijana hao.

“Hii inamaanisha kuwa walikuwa wageni katika maeneo ya mgodi huu, ndiyo maana walikuwa wakiingia shimoni kwa kuvizia.” aliongezea Diwani Seif.

Mbwana alisema kijana aliyenusuruka kuangukiwa na kifusi akiwa na marehemu alipiga kelele ya kuomba msaada kwa wenzao na taarifa zilifika hadi kituo kidogo cha polisi Lukula, ambapo polisi walipofika eneo la tukio walikuta mmoja tayari ameshafariki dunia.

Diwani huyo alisema mwili wa Peter ulisafirishwa kwenda kijijini kwao kwa mazishi.

Kutokana na tukio hilo, diwani huyo alitoa wito kwa wachimbaji katika mgodi huo kuchukua tahadhari na kuzingatia usalama wao katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.

Soma pia:  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Takukuru

Naye, kiongozi anayesimamia masuala ya leseni kwa wachimbaji hao, Abdallah Mlasi, alisema kuwa ndugu wa marehemu walikuwa wilayani Sikonge na waliomba wasaidiwe kuutoa mwili wake kuupeleka kwao na walifanya hivyo baada ya kuchangishana fedha.

Hata hivyo, Kamanda Polisi mkoani Tabora, Wilbroad Mutafungwa, alipotafuta taarifa kuhusiana na suala hilo alisema bado hajapata taarifa kamili na kuahidi kulifuatilia.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories