Michezo

Kauli ya Okwi kwa Simba, Okwi Kujiunga na Fujairah FC

0
Okwi Kujiunga Fujairah FC
Emmanuel Okwi

Sitaisahau Simba! Hayo ni maneno ya mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Uganda (Uganda Cranes), Emmanuel Okwi, ambaye anatarajia kukamilisha mchakato wa kujiunga na klabu ya Fujairah FC inayoshiriki Ligi Kuu Falme za Kiarabu (UAE).

Okwi anajiunga na Waarabu hao akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia Simba ambayo msimu uliopita aliisadia kufika hatua ya robo fainali ya mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mganda huyo ambaye alionyesha kiwango cha juu katika mechi zote nne za Cranes kwenye fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019), amefikia uamuzi wa kuondoka Simba baada ya kuridhika na ofa ambayo ameipata kutoka kwa Fujairah.

Okwi, alisema kuwa anaamini atarejea Tanzania, na atarudi kama mchezaji wa Simba kwa sababu klabu hiyo imemfanyia mambo mengi mazuri.

Soma pia:  Simba, Azam macho yote CECAFA Kagame

Okwi, mshambuliaji wa zamani wa SC Villa ya Uganda, Yanga na Simba alisema kwamba ameishi vema na viongozi, wachezaji na mashabiki wa Simba, hivyo klabu hiyo itaendelea kubakia kwenye kumbukumbu zake nzuri wakati wote.

“Sitaweza kuisahau Simba, ni kama nyumbani, mimi ninaichukulia hivyo, ila maisha ya mpira hubadilika kulingana na wakati, ninahitaji kutumia kila fursa ninayopata, ninawashukuru na nitaendelea kuwashukuru,” alisema mshambuliaji huyo.

Taarifa zilizopatikana jijini zinasema kuwa mazungumzo kati ya Okwi na klabu hiyo ya Uarabuni yako katika hatua za mwisho.

“Mpaka muda huu naweza kukwambia kuwa mazungumzo kati ya Okwi na Fujairah yamefikia zaidi ya asilimia 80, nafikiri hatarudi Simba. Inaonekana msimu huu alitaka kuondoka na kujaribu maisha sehemu nyingine, Afcon alifanya kazi kubwa,” kilisema chanzo chetu.

Soma pia:  Mambo yaiva Simba vs Al Ahly Taifa kesho

Okwi ambaye pia aliwahi kucheza soka la kulipwa Tunisia na Denmark, amekuwa makini zaidi katika suala la usajili na alikataa kusaini mkataba mapema na Simba, akifahamu wazi, thamani yake itaongezea baada ya Afcon.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo