Michezo

Simba, Azam macho yote CECAFA Kagame

0
Simba, Azam macho yote CECAFA Kagame
CECAFA Kagame

Timu za Simba na Azam FC zimeyatolea macho machindano ya Kombe la CECAFA Kagame yanatarajiwa kuanza kesho.

Michuano ya Kombe hilo yataanza kesho kutwa kwenye viwanja vya Taifa Dar es Salaam na Azam Complex, Chamazi. Timu ya Simba itacheza mechi za kundi C kwenye Uwanja wa Taifa wakati Azam FC iliyopo kundi A itacheza michezo yake Uwanja wa Chamazi.

Simba imepata nafasi ya kucheza michuano hiyo kama nafasi ya upendeleo ambayo nchi mwenyeji imekuwa ikipewa huku Azam FC ikicheza kama bingwa mtetezi.

Mabingwa hao wa Ligi kuu Tanzania Bara msimu ilimazika, wamepangwa na timu za Singida united, Dakadaha ya Somali na Saint George ya Ethiopia.

Azam FC imepangwa kundi A itakachuana na timu za KCCA ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC wa Sudan Kusini. Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, alisema kikosi chake bado kinajinoa kwajili ya michuano hiyo.

Soma pia:  TP - Mazembe yahitimisha safari ya Simba CAF Champion League

Alisema kwa sasa anatoa mazoezi maalumu katika kikosi chake ili kufanya vyema kwenye michuano hiyo mikubwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Djuma alisema katika programu yake ya mazoezi atahakikisha anatafuta kikosi kipya cha kwanza kwajili ya michuano hiyo.

Upande wa Azam FC, Ofisa Habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, alisema benchi la Ufundi la timu hiyo kwa ajili ya Fainali za michuano hiyo. Alisema benchi lao la ufundi linatoa mazoezi makali kwajili ya kuhakikisha timu inatwaa ubingwa huo mara nyingine msimu huu.

“Sisi ndio wenye ubingwa tunaamini kwamba tutatetea kwa mara nyingine, kikosi kinafanya mazoezi ya nguvu, naamini tutafanya vyema zaidi ili kuhakikisha tunafikia malengo,” alisema Idd.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo