Top Stories

Botswana inapata Rais mpya leo kufuatia kungatuka kwa Ian Khama

0
Botswana inapata Rais mpya
Rais mpya wa Botswana, Mokgweetsi Maasisi

Leo Jumapili April 8 2018, Botswana inapata  Rais mpya wa tano, Mokgweetsi Maasisi, kufuatia kungatuka kwa Rais wa Serikali ya awamu ya nne, Jenerali Seretse Ian Khama, Jumamosi ya wiki iliyopita baada ya kuwa ofisini kwa miaka 10.

Hata hivyo Masisi aliyekuwa Makamu wa Rais kuanzia mwaka jana, anakuwa rais wa tano kuliongoza taifa hilo tajiri kwa madini ya almasi, lililopo kusini mwa Afrika, anayetoka nje ya udhibiti wa kisiasa wa familia ya hayati Rais Seretse Khama, tangu Uhuru wa nchi hiyo ulipopatikana mwaka 1966.

ian Khama

ian Khama

Ian Khana akiwa na umri wa miaka 55 hivi sasa, kama alivyokuwa Jenerali Khama alipokuwa akiingia oficini mwaka 2008, Masisi anaingia ikulu ili kuingoza Bostwana ambayo inaonekana kuwa alama ya demokrasia barani Afrika na pia inachukuliwa kama mfano wa uimara wa uchumi.

Lakini hatimaye inakabiliwa na ulazima wa kupunguza utegemezi wake wa madini aina ya almasi.

“Sina hakika sana kuhusu uimara wake wa masuala ya uchumi, lakini endapo atateua mawaziri ambao anawaamini hapo anaweza kufikia lengo,” anasema mchambuzi wa masuala  ya kisiasa nchini humo, Ndulamo Anthony Morima.

Masisi ambaye ni mwalimu kitaaluma aliyewahi kufanya kazi katika Mfuko a Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNCF) akiwa ofisa miradi ya elimu kwa miaka minane kuanzia mwaka 1995 hadi 2003, alichaguliwa kuwa mtunga sheria ilipofika mwaka 2009.

Alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Masuala ya Umma) kuanzia mwaka 2011 hadi 2014 alipoteuliwa na Khama kuwa Waziri wa Elimu, nafasi aliyoendelea nayo kwa miaka mitatu mpaka mwaka jana alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Soma pia:  Kampuni kulipwa mafuta kujenga barabara

“Jumuiya ya wafanyabiashara inamwona kama rafiki zaidi wa biashara, hivyo hakuna mashaka kwamba atafanya vizur katika eneo hilo la Uchumi”, anasema Mchumi mwandamizi wa Bostwana, Moatlhodi Sebabole.

Moatlhodi Sebabole ameongezea kwa kusema;

“Anaonekana kuwa atakuja na mikakati mipya na bora zaidi ya kuimarisha shughuli za uchumi”.

Na kama ilivyokuwa kwa Rais wa Serikali ya awamu ya tatu, Festus Mogae na Rais wa Serikali ya awamu ya nne, Luteni Jenerali Seretse Ian Khama, ambaye alingatuka Jumamosi ya wiki iliyopita, Mokgweetsi Maasi naye anaingia ofisini mwaka moja kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Katiba ya Botswana, Rais wa nchi hiyo iliyopo Kusini mwa Afrika anatakiwa kuwepo madarakani kwa vipindi viwili tu vya miaka mitano kila kimoja.

ian Kama Rais wa Botswana

ian Kama

Jenerali Khama, mtoto wa Rais wa Kwanza wa Botswana, Hayati Sir Seretse Khama aliyefariki dunia mwaka 1979, aliingia pia madarakani ikiwa ni mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2009.

Alifanya hivyo kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Festus Mogae ambaye naye alikabidhiwa ofisi kwa namna hiyo na Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili ambaye pia hivi sasa ni hayati, Ketumire Masire mwaka 1998.

Bostwana Ikiwa ni miongoni mwa nchi zilizokuwa ni maskini zaidi duniani katika miaka ya 1970, Botswana ilijigeuza yenyewe na kuingia katika kundi la mataifa yanayopiga hatua kubwa na kwa haraka kabisa kiuchumi hivi sasa.

Soma pia:  Russia yawatimua wanadiplomasia wa Marekani

Kulingana na pato lake la wastani wa dola billioni tatu za Marekani kwa mwaka kutokana na mauzo ya almasi peke yake, nchi hiyo imekuwa ni miongoni mwa zile zinazozalisha kwa wingi aina ya madini hayo duniani, hatua iliyofanyika pia kufikia kipato cha kati kwa wananchi wake.

Hata hivyo, utajiri wa nchi hiyo wa kutegemea zaidi sekta ya madini peke yake, ulitikisa wakati watu takribani millioni mbili walipokosa ajira baada ya soko la madini hayo duniani kuporomoka mwaka 2014, hatua iliyosababisha kushuka kwa uchumi wake kwa muda wa miaka mitatu.

“Anazijua vizuri changamoto zinazoikabili nchi yetu na nina hakika ana uwezo mkubwa wa kupambana nazo”, anasema dereva teksi katika mji mkuu wa Gaborone, Mothusi Sename mwenyewe umri wa miaka 41 wakati akimwelezea rais mpya wa Botswana, Mokgweetsi Masisi.

Je!! Ni mwisho wa Udhibiti wa kisiasa?

Kungatuka Ikulu kwa Rais Seretse Ian Khama, kunamwacha mdogo wake ambaye pia ni Waziri wa Utalii, Tshekedi Seretse Khama akiwa ndiye mwanafamilia pekee ya Rais wa Kwanza wa nchi hiyo, hayati Sir Seretse Khama, akiwa katika nafasi ya juu kiasi hicho ya ndani ya Serikali.

Endapo Masisi hatamteua kuwa Makamu wa Rais, hatua hiyo itakuwa ya kwanza kwa familia hiyo maarufu na inayoheshimika zaidi nchini humo, kutokuwemo katika uongozi wa juu kabisa wa kitaifa.

Luteni Jenerali Seretse Ian Khama, kapera mwenye umri wa miaka 65 anafahamika jinsi anavyoweza kuwashambulia hadharani marais wenzake, baadhi kati yao ni Rais Donald Trump wa Marekani kwa tuhuma za kuwadhalilisha Waafrika alipodai kuwa bara lao ni chafu.

Soma pia:  Putin na Macron wasimamia amani Syria
ian khama mugabe

Rais Mstaafu, Ian Khana akiwa na Rais Mugabe

Kana kwamba haitoshi, hatua hiyo aliwahi pia kuichukua dhidi ya aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alipokwenda kumpokea wakati wa ziara yake nchini humo.

Alizaliwa mjini Chertsey Surrey nchini Uingereza Februari 27 1953, kipindi ambacho baba yake alikuwa amekimbilia taifa hilo la Ulaya ya Magharibi, kisha akaja kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya nne ya Botswana mwaka 2008.

Sir Seretse Khama alifanya hivyo akikwepa asikamatwe na serikali ya kikoloni ya Waingereza haohao wenyewe katika upande wa kwanza, lakini pia aliukimbia utawala wa kibaguzi wa rangi wa makaburu wa Afrika Kusini kutokana na kuoa kwake mwanamke wa mzungu wa Kiingereza aliyeitwa Ruth.

Chama kinachotawala cha Botswana Democratic (BDP) kinatarajiwa kumteua rais mpya anayechukuwa madaraka leo, Jumapili Aprili 8, 2018, Mokgweetsi Masisi ili kugombea rasmi nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka ujao.

Baada ya awali kuwa Mkuu wa Majeshi ya Botswana (BDF), Luteni Jenerali Seretse Ian Khama aliingia kwenye shughuli za kisiasa na kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais kuanzia mwaka 1998 hadi 2008, kisha akamrithi mtangulizi wake katika wadhifa huo, Festus Mogae na kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya tano kuanzia Aprili Mosi, 2008.

Aligombea na kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2009, kisha akashinda tena zoezi hilo ilipofika Oktoba 2014.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories