Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Masuala ya Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) umetoa dola za Marekani milioni mbili kusaidia kujiandaa katika kupambana na virusi vya ugonjwa wa ebola, kwa kuwalenga watu 440,000 walio katika maeneo hatarishi.
Mratibu wa masuala ya kibinadamu Sudan Kusini, Alain Noudéhou, alisema kupitia ufadhili wa mfuko huo shughuli mbalimbali za kupambana na ugonjwa huo zitafanyika. ‘
Alitaja baadhi ya shughuli hizo kuwa zitafanywa katika mipaka na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) pamoja na kuhakikisha kunakuwa na maji safi na salama.
Comments