Top Stories

Treni zagongana Hispania, mmoja afa, 95 wajeruhiwa

0
Treni zagongana Hispania
Ajali ya Treni Spain

Mtu mmoja amekufa na wengine 95 wamejeruhiwa baada ya treni mbili kugongana uso kwa uso mashariki mwa Hispania. Mfanyakazi wa reli ya umma, Renfe Operadora, alisema ajali hiyo ilisababisha kifo cha dereva mmoja wa treni.

Mbali na dereva huyo, wengine 95 walijeruhiwa ambapo watatu kati yao, hali zao ni mbaya. Mmoja wa viongozi katika eneo hilo, Damia Calvet alisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na ubovu wa mfumo wa mawasiliano ambao ungezuia moja ya treni kwenda uelekeo tofauti.

Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo alisema aliiona treni moja ikienda katika njia ambayo siyo yake na dereva hakuwa na muda wa kutosha kuepusha ajali na matokeo yake ziligongana uso kwa uso na kushuhudia vioo vikipasuka na kurushwa eneo la tukio.

Soma pia:  Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu kuokotwa kwa mwili wa mmiliki wa Super Sami

Waziri Mkuu wa Hispania, Pedro Sanchez alituma salamu zake za rambi rambi kwa familia ya marehemu na salamu za pole kwa majeruhi.

Imeelezwa Novemba 20, 2018, treni iliyokuwa imebeba watu 133 ilipata ajali katika njia hiyo hiyo kutokana na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa na kuua mtu mmoja na kujeruhi watu wengine 50.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories