Top Stories

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu kuokotwa kwa mwili wa mmiliki wa Super Sami

0
kuokotwa kwa mwili wa mmiliki wa Super Sami
mmiliki wa Mabasi ya SuperSami

Jeshi la Polisi mkoani Mara, limetoa taarifa rasmi juu ya kuokotwa kwa mwili wa Mfanya biashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah , ambaye alitoweka na mwili wake kuokotwa mtoni hapo juzi pamoja na Gari lake kuchomwa moto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Jafari Mohamedi, amesema hapo Jumatano walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuokotwa kwa kiroba chenye mwili ndani, na walipokifungua na kuita watu ili kuutambuwa mwili huo, ndipo walipokugundua kuwa ni mwili wa Mfanya biashara huyo anayeishi mkoani Mwanza.

“Jumatano jioni tumeweza kupata mwili wa marehemu huyu Samson Josiah ambaye ni mmiliki wa mabasi ya Super Sammy anayeishi Mwanz. Tulipata taarifa kwamba kuna mwili umeonekana katika mto ambao unatenganisha mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu unaoelekea mbugani Serengeti, wananchi waliona kiroba kimefungwa kinaelea, kikavutwa wakajulishwa polisi kufungua ndani wakakuta mwili wa marehemu”. alisema Kamanda Mohamedi.

Soma pia:  Treni zagongana Hispania, mmoja afa, 95 wajeruhiwa

Vilevile kamanda Mohamedi aliongezea kwa kusema” Kwa sababu tulikuwa na taarifa za utafutaji na mashaka juu ya kutoweka kwake, tukajulisha ndugu hao na wakatambua mwili wa marehemu”.

Kamanda Mohamedi alisema kuwa Marehemu alitoweka kuanzia tarehe 27 mwezi wa Februari ambapo aliondoka mkoani Mwanza, na ndugu zake walisema kuwa aliaga anaenda Simiyu kwa shughuli zake za kibiashara, tangu siku hiyo hakuonekana tena, na gari yake aliyotoka nayo Mwanza kukutwa imechomwa moto maeneo ya Serengeti mnamo tarehe 8 hadi kuteketea.

Imeelezwa kwamba kwa sasa mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya postmoterm, na baadaye utatolewa kwenda kuzikwa, na mpaka sasa watu wanne wameshikiliwa kufuatia tukio hilo, upelelezi bado unaendelea.

mwili wa mmiliki wa Super Sami
mwili wa mmiliki wa Super Sami

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories