Michezo

Arsene Wenger kufanya usajili

0
Arsene Wenger kufanya usajili
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kufanya usajili ili kuimarisha kikosi chake na kuongeza nguvu baadhi ya wachezaji.

Kocha huyo amesema kuwa amepanga kusuka kikosi chake kwa kusajili baadhi ya wachezaji hasa kwenye nafasi ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.

Wenger amesema hayo wakati akizungumza na gazeti moja la nchini England kuwa kikosi chake kina matatizo kwenye sehemu hizo.

“Nataka nisajili mlinzi wakati, kiungo na washambuliaji ili kuongeza nguvu katika timu yangu,” alisema Arsene Wenger.

Hatua hiyo, huenda ikawa ni kutaka kuziba nafasi ya Jack Wilshere ambaye huenda akaondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu.

Siku ya kesho Arsenal itapambana na Stock city majira ya saa 9:30 jioni wakiwa nyumbani katika Uwanja wa Emirates.

Soma pia:  Real Madrid wakomaa na Pogba

Comments

Comments are closed.

More in Michezo