Top Stories

Walimu watishia Mgomo waliohamishwa kutoka shule ya Sekondari na kwenda shule ya msingi

0
Walimu waliohamishwa kutoka shule ya Sekondari
Mkurugenzi wa Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda

Sakata la Walimu waliohamishwa kutoka shule ya Sekondari na kwenda shule ya msingi kufundisha masomo ya sanaa, limechukua sura mpya, baada ya kudai kutoridhishwa na majibu ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, aliyokuwa ameahidi kuwasikiliza na badala yake wamedai wanashinikiza mgomo wa kutofundisha.

Wakizungumza baada ya Mkurugenzi wa Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda, kukutana na walimu hao kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) mjini Njombe, walisema majibu aliyowapatia kuhusu madai hayo hayakujitosheleza na kwamba hawatakwenda ngazi ya juu.

Mariam Mligo, mmoja wa walimu hao, alisema walitarajia kupata majibu ya lini stahiki zao wanazodai watalipwa, lakini Mkurugenzi huyo alishindwa kuwapatia majibu na badala yake aliwataka warudi kwenye vituo vyao vya kufanyia kazi.

Soma pia:  Mgomo Makerere bado moto

“Yeye kama kiongozi alitakiwa kutusikiliza au kujibu zile hoja ambazo sisi tulimueleza na kwamba yeye ndiye aliyetoa wito tukutane leo (juzi), tulikuwa tnajua tutapata majibu mawili ama kulipwa stahiki zetu au kurudishwa katika vituo vya awali.

“Lakini cha ajabu tumeletewa askari polisi, zaidi amekuja hapa akatueleza hataki maswali, yeye demokrasia kwake haijawahi kutokea,” alisema Mariam.

Mwalimu huyo alisema watakwenda kwenye maeneo ya vituo vya kazi, lakini hawako tayari kuendelea kufanya kazi.

“Sisi kama walimu tunachosema, mimi nawakilisha walimu wote wa halmashauri ya Mji wa Njombe, hatutafanya kazi yoyote kuanzia sasa hivi, vituo hivyo tutalipoti kuanzia sasa hivi, lakini kama yeye anahitaji kuona tunaripoti bila kufanya kazi yoyote,” alisema Mariam.

Akizungumzia madai hayo kwa niaba ya Mkurugenzi, Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji haina bajeti itakayotosheleza kulipa stahiki za walimu hao kwa wakati.

Soma pia:  Historia ya Intaneti, Mambo 16 huenda ulikuwa huyajui kuhusu Intaneti

“Fedha ambazo tunasema zitumike za P4R hazikidhi mahitaji ya kuweza kuwalipa walimu wote kwa wakati mmoja, kwenye halmashauri yetu ya Mji Njombe fedha za uhamisho ambazo zinaitwa P4R kwa kipindi hiki tumeletewa milioni 17.4 na ili tuweze kukidhi malipo ya walimu wote  tunahitajika tuwe na Sh. milioni 225,” alisema Mbujilo.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Walimu Wilaya ya Njombe, Salama Lupenza, alisema watawasilisha malalamiko ya walimu hao ngazi ya juu ili wasikilizwe.

“Mkurugenzi bado anasimama na msimamo kwamba hana hela ya kutosha ya kuwalipa sasa hivi, kwa hiyo kama chama tumona sasa tufike hatua tupeleke ngazi ya mkoa ili mkoa nao kwa nafasi yake usaidi,” alisema Salama

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories