Burudani

Waandaaji Grammy wazua jambo

0
Waandaaji Grammy wazua jambo
Drake akiongea baada ya kuchukuwa tuzo za Grammy

Tuzo za Grammy zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita bado zimeendelea kutengeneza habari mpya lakini zikiwa za kukosolewa zaidi baada ya kuelezwa kushindwa kutoa tiketi mbili za 21 Savage na mama yake huku wakiliacha jina la marehemu XXXTentacion katika ibada maalum ya kuwaombea marehemu kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.

21 Savage ambaye kwa sasa yupo lupango kutokana na kesi ya masuala ya uraia wake inayomuandama alikuwa akiwania tuzo mbili na alishawekwa kwenye orodha ya watakaotumbuiza siku hiyo lakini meneja wake alipofuatilia kuhusu tiketi hizo, waandaaji hawakuwa na jibu la maana zaidi ya kusema Savage yupo kwenye masuala ya siasa kwa sasa na wao hawataki kujihusisha nayo.

Upande mwingine, imefafanuliwa kuwa waandaaji wa Grammy waliwaombea marehemu wawili tu; Mac Miller na DJ Avicii.

Soma pia:  Drake: God's Plan (Official Video)

Walipoulizwa kuhusu XXXT walijitetea kuwa aliachwa kutokana na kuwahi kuwa mtu wa vurugu na uhalifu.

Kabla ya hapo, waandaaji wa tuzo za Grammy ambao wamekuwa wakishutumiwa kwa vitendo vya ubaguzi walidaiwa kumzimia Drake kipaza sauti wakati akizungumza baada ya kushinda tuzo yake ya wimbo bora wa rap.

Drake alisema: “Tambua tayari umeshinda kama una watu ambao wanaimba nyimbo zako neno kwa neno, kama kuna watu wavuja jasho wanakuja kununua tiketi za tamasha lako basi uhitaji kuwa na hii hapa (tuzo), wewe tayari umeshinda,”.

Hata hivyo waandaaji wa Grammy wamesema hawakuzima makusudi, walidhani Drake amemaliza kuzungumza.

Comments

Comments are closed.

More in Burudani