Michezo

Waafrika 10 watakoiwakilisha Ulaya Kombe la Dunia

0

Wakati Mashindano ya Kombe la Dunia ya Mwaka 2018 yakikaribia kuanza nchini Russia, baadhi ya wachezaji wa Ulaya wanaotarajiwa kungara kwenye mashindano hayo wana asili ya Bara la Afrika.

Hawa ni miongoni mwa Waafrika watakoiwakilisha Ulaya Kombe la Dunia 2018:-

1) Christian Benteke

Christian Benteke
Christian Benteke

Benteke aliwasili nchini Ubelgiji akiwa mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo mwaka 1993; kipindi ambacho dikteta Mobutu Sese Seko, alipokuwa akitawala taifa hilo.

Alizaliwa Kinshasa mwaka 1990, na kufanikiwa kuiwakilisha Ubelgiji mwaka 2007 kwenye mashindano ya FIFA ya Vijana walio chini ya umri wa miaka 17.

2) Paul Pogba

Paul Pogba
Paul Pogba

Kiungo huyu wa Ufaransa alizaliwa katika jiji la Siene-et-Marne, France na wazazi wake raia wa Guinea. Alianza kuchezea timu ya taifa ya vijana Les Bleus akiwa na umri wa miaka 16, chini ya kocha Guy Ferrier.

Soma pia:  Je Wajua? Wamakonde ndio walioanzisha Msasani

3) Divock Origi

Divock Origi
Divock Origi

Origi ni mtoto wa aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Kenya, Mike Origi. Alizaliwa Ostend, Ubelgiji na kukulia Houthalend-Oost.

Origini mwenye umri wa miaka 22 sasa aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Ubelgiji cha Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2014, na tangu wakati huo ameichezea timu ya taifa hilo mara 23 na kufunga magoli matatu

4) Luis Nani

Luis Nani
Luis Nani

Winga huyu wa Ureno asili yake ni Cape Verde. Aliletwa Ureno baada ya kutelekezwa na wazazi wake. Baba alimwacha akiwa na umri wa miaka mitano, alikwenda likizo Cape Verde, na tangu wakati huo hakurejea tena Ureno.

5) Marouane Fellaini

Marouane Fellaini
Marouane Fellaini

Kiungo huyu wa Ubelgiji alizaliwa na wazazi wake kwenye wenye asili ya Morocco na akakulia brussels, Ubelgiji. Baba yake Abdellatif, ni kipa wa zamani wa miamba ya soka Raja Casablanca ya Morocco.

Soma pia:  Top 10 ya Nchi tajiri Afrika kwa GDP

Fellaini ni miongoni mwa wachezaji watakaoiwakilisha Ubelgiji kwenye Kombe la Dunia nchini Russia

6) Dele Alli

Dele Alli
Dele Alli

Mchezaji wa Kimataifa, alizaliwa na baba raia wa Nigeria anayeitwa Kenny na mama raia wa Uingereza, Denise.

Mwaka 2015, alikataa ofa ya kuichezea Nigeria na akaitwa kwenye kikosi cha Uingereza kwenye mashindano ya kufuzu EURO mwaka 2016 dhidi ya Estonia na Lithuania.

7) N’Golo Kante

N'Golo Kante
N’Golo Kante

Kiongo huyu wa Ufaransa alizaliwa na wazazi wenye uraia wa MAli. Mwaka 2015 aliombwa na taifa hilo ashiriki kwenye timu ya taifa kwenye mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika.

Hata hivyo, alikataa na kwa mara nyingine Mali ilimwomba mwaka 2016, pia alikataa. Badala yake akakubali maombi ya kuichezea Ufaransa.

Soma pia:  Mambo 10 huenda ulikuwa huyafahamu kuhusu Ronaldo

8) Eder Lopez

Eder Lopez
Eder Lopez

Anakumbukwa kwa kufunga goli la ushindi la Ueno kwenye fainali za Kombe la Ulaya mwaka 2016 nchini Ufaransa.

Eder alizaliwa Bissau, Guinea-Bissau na alihamia nchini Ureno akiwa bado mtoto na kuanza kucheza soka akuwa na umri wa miaka 11 katika akademi ya Associacao Desportiva e Cultural da Ademia.

9) Sami Khedira

Sami Khedira
Sami Khedira

Mjerumani huyu alizaliwa na baba raia wa Tunisia na mama raia wa Ujerumani.

Alichaguliwa kuichezea Ujerumani kwenye mechi ya kirafiki ya maandalizi ya Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2009 dhidi ya Afrika Kusini.

10) Blaise Matuidi

Blaise Matuidi
Blaise Matuidi

Kiungo huyu wa Ufaransa baba yake, Faria Rivelino, ni raia wa Angola, alienda Ufaransa akiwa bado mtoto mdogo, Mama yake Elisse ni Mzaliwa wa Congo.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo