Burudani

Usher na Rich the Kid wavamiwa studio

0
Usher na Rich the Kid wavamiwa studio
Usher na Rich the Kid

Kizazaa kiliibuka juzi katika Studio za Westlake Recording baada ya watu wasiojulikana kuvamia katika eneo la nje la jengo hilo na kuanza kufyatua risasi kwa lengo la kuwaibia wanamuziki waliokuwa hapo; Usher Raymond na Rich the Kid.

Inaelezwa kuwa wakati risasi zikiendelea kurindima, Usher alikuwa ndani akirekodi na kulazimika kusitisha zoezi hilo wakati Rich na rafiki zake waliokuwa nje walinusurika kupigwa risasi kabla ya kuporwa pesa taslimu na vito vya thamani.

Ripoti zinaeleza kuwa licha ya wezi hao kuondoka na polisi kutanda eneo hilo lakini Usher hakutoka ndani mpaka usiku aliposikia hali ni shwari kabisa na alipojaribu kuhojiwa hakutaka kueleza chochote kuhusiana na hilo.

Hii ni mara ya pili, Rich anavamiwa na kuporwa mali zake, polisi wa eneo hilo wanaendelea na uchunguzi wa kina kubaini juu ya matukio hayo yanayohatarisha amani kila kukicha.

Soma pia:  Waandaaji Grammy wazua jambo

Video ya tukio

Comments

Comments are closed.

More in Burudani