Burudani

Simanzi, Kifo cha Godzilla

0
Kifo cha Godzilla
Mwana Hip Hop, Godzilla

Msanii wa muziki wa hip hop, Golden Mbunda ‘Godzilla’ amefariki jana alfajiri na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa dada yake Joyce Mbunda, Godzilla alianza kuugua ghafla, presha ilishuka na sukari ilipanda pamoja na kuumwa na tumbo kabla ya kuaga dunia jana alfajiri.

“Ni kweli amefariki na chanzo cha kifo kimetokana na kuugua ghafla akiwa nyumbani na mipango ya mazishi inafanywa nyumbani Salasala,” alisema dada yake huyo.

Godzilla wakati wa uhai wake alijizolea umaarufu kupitia muziki wa hop hop, wimbo wake wa Lakuchumpa aliomshirikisha Joti ulihit zaidi Tanzania pamoja na nyimbo zingine ‘Nataka’ na ‘King Zilla’, na pia kwa uwezo wake wa kughani mashairi papo kwa papo kwa njia ya freestyle.

Soma pia:  Mwili wa Emiliano Sala wapatikana

Alizaliwa Januari 5, 1988 mkoani Morogoro. Alitambulika katika tasnia ya muziki kwa wimbo wake ulioitwa ‘Salasala’, ambao pia unatambulisha mtaa wake aliokuwa akiishi.

Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.

https://www.youtube.com/watch?v=RtkTt58t0RA
Lakuchumpa

Comments

Comments are closed.

More in Burudani