Michezo

Sarri ataka Juventus imsajili Danny

0
Sarri ataka Juventus imsajili Danny
Danny Rose

Kocha wa Juventus, Maurizio Sarri ameitaka klabu yake kumsajili nyota wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Danny Rose.

Sarri amewaambia waajiri wake hao wapya kuhakikisha wanamsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, kwani alikuwa akimfuatilia hata wakati akiinoa Chelsea.

Spurs ipo tayari kumuuza beki huyo wa pembeni kipindi hiki cha majira ya joto baada ya kumuuza, Kieran Trippier aliyetua Atletico Madrid kwa pauni milioni 20.

Usajili wa Trippier ulikamilika kabla ya Spurs kupaa kwenda nchini Singapore na Rose aliachwa kwenye kikosi hicho cha kocha Mauricio Pochettino wakati akisubiria hatima yake.

Sarri anahisi kwamba ana nafasi kwenye kikosi chake kwa beki wa kushoto, huku mchezaji Luca Pellegrini aliyesajiliwa hivi karibuni akitarajiwa kupelekwa kwa mkopo kule Cagliari.

Soma pia:  Manchester United yakaribia kumsajili Dybala

Na sasa Sarri anataka kuhakikisha kwamba klabu yake inafanya jitihada za kumsajili Rose ambaye pia amekuwa akiwaniwa na Klabu ya Paris Saint Germain na miamba wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Schalke.

Spurs inapanga kumsajili nyota wa Fulham, Ryan Sessegnon ambaye ndiye atakuwa mbadala wa Rose na tayari wameshafikia makubaliano binafsi ya kutua hapo London Kaskazini.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo