Burudani

Samia Suluhu na Kikwete kuguswa na Kifo cha Godzilla

0
Kifo cha Godzilla
Rapa Godzilla

Makamu wa Rais Samia Suluhu ameguswa na msiba wa msanii wa Hip Hop Golden Jackob ‘Godzillah’ aliyefariki usiku wa kuamkia juzi.

Akizungumza kwenye kongamano la dawa za kulevya Samia Suluhu aliwaomba watu kusimama kwa dakika moja kumuombea Godzillah.

“Nimepata taarifa kuwa usiku wa kuamkia leo (juzi) tumepata msiba wa msanii mmoja ambaye naye ni ndugu yetu Golden Jacob Mbunda kwa umaarufu anajulikana kama Godzillah amefariki, sasa naomba wote tusimame kwa dakika moja tumpe heshima yake na kila mmoja aombe kwa kitabu anachokiamini,” alisema Samia.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais mstaafu Jakaya Kikwete ameonyeshwa kuguswa na msiba huo na kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu.

“Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha msanii wa kizazi kipya Godzilla, alikuwa kijana mdogo mwenye ndoto kubwa na amedondoka wakati ambapo bado mchango wake unahitajika,nawapa pole familia ya marehemu,”alisema Kikwete.

Godzillah alifariki usiku wa kuamkia juzi nyumbani kwao Mbezi Salasala baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Soma pia:  Simanzi, Kifo cha Godzilla

Comments

Comments are closed.

More in Burudani