Top Stories

Rabbi wa Israel kuwakashifu Waafrika

0
Israel kuwakashifu Waafrika
Rabbi wa Israel

Shirika la haki za Binaadamu na Mshikamano na Palestina nchini Afrika Kusini, limelaani vikali matamshi ya kibaguzi yaliyotolewa na kiongozi mkuu wa Uyahudi nchini Israel, Yitzhak Yosef.

Kiongozi huyo hivi karibuni katika video iliyorushwa na kituo cha habari cha Israel, Ynet News amenukuliwa akiwafananisha Waafrika na ‘Nyani’, huku akitumia neno “Kuchi” kuwaita watu weusi, neno ambalo kwa mujibu wa lugha ya Kiibrania ya kisasa, hutumika kuwadharau watu wenye rangi nyeusi.

Hii sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kutumia mamlaka yake kuhalalisha ubaguzi kwani katika hotuba yake aliyotoa mnamo mwezi Mei mwaka uliopita, alinukuliwa akisema wasichana wanaofuata usekulari wanatabia kama za Wanyama kutokana na jinsi wanavyovaa huku Machi 2016 alisema kwamba wasiokua mayahudi hawapaswi kuishi Israel.

Soma pia:  Russia yawatimua wanadiplomasia wa Marekani

Mtazamo wa Kiongozi huyo ni mbaya hususani katika ubaguzi unaoendelea kuenea dhidi ya Waafrika na watu wenye asili ya Palestina.

Hivi karibuni serikali ya Israel imeendelea kuwafukuza maelfu ya Waafrika ambapo wanatakiwa kuondoka Israel kabla ya mwezi Aprili mwaka huu na kwamba asiyetii amri hiyo atakwenda jela.

Pamoja na hayo, Israel imetoa kiasi cha randi laki moja kwa yeyote atakaesaidia kukamatwa na kufukuzwa kwa nguvu Waafika wanaotaka hifadhi nchini humo.

Waziri mkuu wa Israel
Benjamin Netanyahu

Viongozi wa Israel wamekuwa wakitoa matamshi ya kibaguzi dhidi ya Waafrika na pia imekuwa ikiwaona Waafika wasiokuwa Wayahudi kama tatizo kwa taifa hilo huku Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu mara kwa mara amekuwa akidai kuwa Waafrika ni tishio kwa jamii yao, hivyo wanapaswa kufukuzwa nchini humo.

Soma pia:  Kampuni kulipwa mafuta kujenga barabara

Kwa upande wake Waziri wa ndani wa Israel, Eli Yishai amenukuliwa akisema: “Wahamiaji wa Kiafrika wanafikiri kwamba nchi hii sio yetu, watu weupe.”

Naye Waziri wa Utamaduni na Michezo wa Israel amewahi kunukuliwa akiwafananisha Waafika na ugonjwa hatari wa saratani. Mnamo mwaka 2013, serikali ya Israel iliripoti kuwafunga uzazi wanawake wa Kiafrika bila ya ridhaa zao.

Comments

Comments are closed.

More in Top Stories