Michezo

Paul Pogba atamani kukipiga na Neymar

0
Paul Pogba atamani kukipiga na Neymar
Paul Pogba

Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amesema ndoto yake ni kuona siku moja anacheza na Straika wa Paris Saint-Germain, Neymar Jr.

Neymar Jr.
Neymar Jr.

Mfaransa huyo ameyaeleza hayo katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na kituo cha televisheni ya Argentina, TyC Sports ambapo alionyeshwa kipande cha nukuu ya Neymar akisema; “Napenda namna alivyo na wakati fulani tunaenda kucheza pamoja,”.

Pogba akajibu kwa kusema; “Ndiyo, ninampenda Neymar. Kwa Brazil, Soka ni kila kitu. Ni maisha ya Brazil kila mmoja anacheza soka, Ninapenda kumuona Neymar akiwa uwanjani.

“Napenda kumuona uwanjani anacheza, kwa ujuzi na ufundi wake. Ni staili tofauti. Unaposema neno Neymar duniani, kila mmoja anafahamu huyo ni nani na anafanya nini. Pamoja na hayo kama nitacheza naye siku moja itakuwa safi.” Paul Pagba alisema

Chris Waddle
Chris Waddle

Vilevile nyota huyo wa Man United anasema kwamba wakatiwa makuzi yake alikuwa anampenda mchezaji wa zamani wa kimataifa wa England, Chris Waddle.

Soma pia:  Pogba amesema hana tatizo na Mourinho

Kwa sasa Paul Pogba hana wakati mzuri sana Old Trafford na kocha, Jose Mourinho amekuwa akimweka benchi Mfaransa huyo kwenye mechi kandaa muhimu.

Paul Pogba anatarajiwa kutumia michezo hii ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Colombia na Urusi ili aweze kurejesha hali yake ya kujiamini.

Paul Pogba
Paul Pogba
Paul Pogba
Paul Pogba

Comments

Comments are closed.

More in Michezo