Michezo

Manchester United kutinga nne bora

0
Manchester United kutinga nne bora
Paul Pogba

Manchester United imesogea mpaka kwenye nafasi nne bora baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fulham jana ugenini Craven Cottage.

Anthony Martial alikuwa kwenye kiwango kizuri, akitengeza bao la kwanza lililofungwa na Paul Pogba (pichani) dakika ya 14 na kufunga bao la pili katika dakika ya 23.

Matokeo ya jana yameifanya United kupata ushindi wa 10 katika mechi 11 ilizocheza chini ya kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer.

Pogba alifunga bao katika kipindi cha pili dakika ya 65 kwa mkwaju wa penalti baada ya Juan Mata kufanyia madhambi eneo la hatari.

Licha ya kufanya mabadiliko kwenye ulinzi, walikuwa kwenye mashaka na Fulham ambayo sasa imeruhusu kufungwa mabao 58 msimu huu na wako kwenye ukanda wa kushuka daraja.

Soma pia:  Guardiola amtetea Sarri na kipigo

United baada ya matokeo ya jana, imepanda kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Chelsea yenye pointi 50.

Man United 3-0 dhidi ya Fulham
Man United washerekea baada ya Ushindi wa jana dhidi ya Fulham

Comments

Comments are closed.

More in Michezo