Michezo

Ozil na Sanchez kwenda Man City

0
Ozil na Sanchez
Ozil na Sanzhez

Kuna tetezi nyingi zinasamba mitandaoni kuhusiana na Uhamisho, mwezi huu.

Inasemekana kuna uwezekano mkubwa sana Alexis Sanchez kuuzwa mwezi huu wa Januari.

Wakati kulikuwa na maslahi kutoka Paris Saint-Germain na Bayern Munich, Manchester City wamejitokeza na imetoa bonus kubwa ya kumsaini kwa mpango wa miaka mingi.

Hatua ambayo ilitarajiwa kufanyika mwisho wa msimu huu lakini kutokana na jeraha la hivi karibuni kwa Gabriel Jesus limefungua mlango, usajili huo kufanyika Januari.

Arsenal itastahili kufanya maamuzi kama watakubaliana na ada ya uhamisho au kumwacha aondoke huru bila ya ada ya Uhamisho, mwisho wa msimu huu.

Mchezaji mwengine mwenye jina kubwa katika Klabu ya Arsenali, Mesut Ozil ambaye mkataba wake unakaribia kuisha msimu huu, huku kuna uwezekano mkubwa wa kumkuta Ozil akijiunga na Man United na kuchezea  kwenye uwanja wa Old Trafford, kwajili Ozil anapendelea kuchezea Ligi kuu ya Uingereza, hasa baada ya Barcelona kumsajili Philippe Coutinho imepelekea kuwa na uwezekano ndogo kuchezea Camp Nou.

Soma pia:  Arsenal, Everton kumgombania Andre Gomes

Pia kuna tetezi kuhusiana na Ozil kujiunga Juventus ama Inter milan, lakini kuna uwezekano mdogo sana Ozil kuchezea ligi ya Italia (Seria A) kwani hawataweza kumpa kiwango cha mshahara anachohitaji yeye kulipwa.

Comments

Comments are closed.

More in Michezo