Benki Kuu nchini hapa wiki hii itatangaza na kutoa noti mpya za faranga 500 na faranga 1,000 zilizotengenezwa kwa gharama ya faranga bilioni tano.
Gavana wa Benki Kuu, John Rwangombwa alisema hatua hiyo ni agizo la rais kutoa noti hizo mpya zitakazogharimu serikali faranga bilioni 1.6 kwa mwaka katika miaka mitatu ijayo.
Kuhusu rangi, faranga 500 mpya itakuwa na rangi ya kahawia wakati ya sasa ina rangi ya bluu huku faranga 1,000 itabaki na rangi hiyo ya bluu.
Noti hizo mpya pia zimeboreshwa katika muundo kutofautishwa kati ya noti hizo mbili zilizotajwa kama changamoto kwa watumiaji pamoja na kuwa na alama maalum ya asili ya Rwanda.
Mchakato wa kutengeneza noti hizo ulifanyika kwa kutangaza zabuni ambayo kampuni ya Ujerumani ya G+D ilishinda kutengeneza noti hizo mbili kwa gharama ya faranga bilioni tano katika miaka mitatu.
Gavana alieleza kuwa kubadilishwa kwa noti hizo kulifanyika kutokana na mfanano kati ya noti hizo, hivyo kuwa vigumu kuzitofautisha.
Comments