Burudani

Nicki Minaj na Young Money wajiondoa tuzo za BET

0
Nicki Minaj tuzo za BET
Nicki Minaj na Cardi B

Nicki Minaj na Lebo ya Young Money wametangaza kutoshiriki tena kwenye tuzo za BET zinazotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu pamoja na kutumbuiza kwenye onesho la BET Experience, mwaka huu.

Nicki ameamua hivyo baada ya chapisho lililowekwa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter wa kituo hicho cha televisheni kuashiria dharau na kashfa kwake hasa baada ya Cardi B kushinda tuzo ya Grammy juzi ikiwa ni mwanamke wa kwanza kushinda kipengele cha albamu bora ya rap tangu kuanzishwa kwa Grammy.

Chapisho hilo ambalo liliambatana na picha ya Cardi, liliandikwa: “Wakati huu, Nicki Minaj amevutwa mzima mzima na wigi lake”.

Hilo limemgusa Nicki na kuamua kuchukua uamuzi huo mgumu.

Soma pia:  Ifahamu filamu ya Armageddon (1998)

Comments

Comments are closed.

More in Burudani