Baraza Kuu la Mitihani nchini Tanzania, NECTA, leo januari 30, 2018, limetangaza rasmi matokeo ya kidato cha nne 2017.
Katibu Mkuu wa NECTA, Dkt Charles Msonde amesema kuwa ufaulu wa ujumla kwa watahiniwa wa kidato cha nne 2017 umeongezeka kwa asilimia 7.22%, kutoka asilimia 70.35% mwaka 2016, kuwa asilimia 77.57% mwaka 2017.
Katika matokeo hayo, Shule 10 zilizoongoza ni:-
- St. Francis Girls – Mbeya
- Feza Boys – Dar es Salaam
- Kemebos – Kagera
- Bethel Sabs Girls – Iringa
- Anwarite Girls – Kilimanjaro
- Marian Girls – Pwani
- Kannosa – Dar es Salaam
- Feza Girls – Dar es Salaam
- Marian Boys – Pwani
- Shamsiye Boys – Dar es Salaam
Kwa upande mwengine, Shule 10 zilizofanya vibaya zaidi ni:-
- Kusini – Kusini Unguja
- Pwani Mchangani – Kaskazini Unguja
- Mwenge S.M.Z – Mjini Magharibi
- Langoni – Mjini Magharibi
- Furaha – Dar es Salaam
- Mbesa – Ruvuma
- Kabugaro – Kagera
- Chokocho – Kusini Pemba
- Nyeburu – Dar es Salaam
- Mtule – Kusini Unguja
Aidha, Dkt Charles Msonde, amesema kuwa “NECTA imefuta matokeo ya watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani huu wa kidato cha nne 2017.”
Kuona matokeo hayo Bofya Hapa.
Comments