Burudani

Mashabiki wamtibua Davido

0
Mashabiki wamtibua Davido
Davido

Nyota wa muziki nchini Nigeria David Adeleke ‘Davido’ amewashukia mashabiki wake wanaomtaka aachane na siasa kwa kuwambia kuwa ana nguvu ya kuzungumzia mambo yote yanayoonekana hayapo sawa kwenye jamii.

Davido kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter alisema kuna watu wanamshauri asijihusishe na siasa lakini yeye amekataa kufanya hivyo akiamini kuwa ana sauti kubwa kutetea maovu kwenye jamii yake.

“Sisi sio tu waburudishaji ila nimechoka na watu kusema tukae mbali na siasa kwa sababu ni hatari, tuna nguvu na wananijua vizuri, ni nchi yetu na kazi yetu kuona jinsi gani nchi inaendeshwa,” alisema Davido.

Soma pia:  Rapper Jay Z si mwaminifu kwa Beyonce

Comments

Comments are closed.

More in Burudani