Burudani

Drake kutengeneza kava la simu milioni 920

0
Drake kutengeneza kava la simu
Drave na Kava hio ya simu yake

Rapa maarufu zaidi nchini Marekani Drake, ameshika headline nyingi kimataifa hivi juzi baada ya kutumia pesa nyingi kutengeneza kava la Simu yake aina ya iPhone.

Drake anafahamika kuwa ni miongoni mwa watu wanaopenda kutumia vitu vyenye thamani kubwa ya zaidi ya fedha kama vile saa za gharama, magar, nyumba za kifahari, n.k.

Mwanamuziki huyo kutoka Young Money ametengenezesha kava la simu yake aina ya iPhone lenye thamani ya Dola za Marekani 400,000 (zaidi ya sh milioni 920).

Imeelezwa kwamba kava hilo limekuwa na gharama kiasi hicho kutokana na kutengenezwa kwa vipande vya almasi yenye gramu 16 huku nyuma ikipambwa kwa chapa ya OVO inayowakilishwa na ndege aina ya Bundi

Soma pia:  Pierre Liquid kula shavu Marekani

Comments

Comments are closed.

More in Burudani